NA DIRAMAKINI
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA), Mhandisi Modestus Lumato amewataka watendaji wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira nchini kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na EWURA ili kuboresha huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika maeneo yao.

“Kama mlivyoelekezwa awali, kuja na mikakati yenu inayozingatia miongozo iliyotolewa na EWURA, mafunzo haya yatawawezesha kuboresha mikakati hiyo itakayoongeza ufanisi wa utendaji wenu,”amesisitiza Mhandisi Lumato.
Naye Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira EWURA, Mhandisi Exaudi Fatael, ameeleza kuwa, EWURA imeandaa miongozo husika kwa lengo la kuimarisha huduma hususani katika kudhibiti majanga.
Sambamba na kudhibiti upotevu wa maji pamoja na namna bora ya kuchagua, kufunga, kupima na kutunza dira za maji ikiwemo muongozo wa kushindanisha utendaji wa mamlaka za maji.
Mafunzo hayo yamewakutanisha watendaji kutoka mamlaka za maji 31ikijumuisha mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Tabora,Singida,Iringa, Kilimanjaro, Tanga, Manyara na Morogoro.