Baba wa Salumu aliyefahamika kama Abdalla Lilingani kwa asili ni jamii na watu wanaotokea huko Nyasa, Malawi ya sasa.
Alitoka huko Nyasa na kufika Rufiji kutafuta maisha, hilo ni jambo la kawaida sana sana kama ilivyo kwa vijana wengi wa leo hii.
Alipofika Rufiji alikaa hapo akaoa mwanamke wa Kirufiji, inavyoonekana Abdalla Lilingani alimzaa Salumu Lilingani kwa mwanamke wa Kinyasa ambaye familia hii haina kumbukumbu zake.
Akiwa Rufiji Abdallah Lilingani alioa mwanamke mwingine wa Kirufiji, maisha ya ndoa yalianza huko mke wa Abdalla akimlea Salumu Abdallah huko huko Rufiji.
Abdallah Lilingani alikaa Rufiji kwa kipindi kifupi sana akaambiwa kuwa anaweza kwenda Tanga kutafuta maisha, maana alijulishwa kuwa huko kuna kazi nyingi zinaweza kumuingizia fedha.
Kumbuka msomaji wangu Salumu analelewa ujomba wa kambo, jambo hili linaweza kuwa geni sana kwa jamii ya leo, lakini Salumu alipata ngekewa hiyo.
Mtu kwao akiwa likizo alikuwa akirudi nyumbani kwao Tanganyika na kwa kuwa Rufiji ni mbali na Dar es Salaam alikuwa kila akifika Tanganyika alinunua nyumba, viwanja kadhaa na mashamba mengi likiwamo shamba lililopo katikati ya Mbagala Kizuiani-Mangaya-Kizinga jirani na shule ya Msingi Mbagala.
Tanganyika ikapata mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kati na mradi huo ulikamilika vizuri.
Salumu sasa ni kijana mkubwa anayejitambua vizuri, huku akiwa na elimu mbalimbali kutoka kwa wamisionari hao waliomchukua kutoka Rufiji.