Kamati ya Bunge yaridhishwa na ujenzi Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP)

NA MWANDISHI WETU 

KAMATI ya Kudumu ya Nishati na Madini imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi Mkubwa wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere Hydropower Project ambao unatekelezwa na Serikali kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme nchini.
Sehemu ya mradi wa JNHPP ambapo maji yatapita kwenda kuzalisha umeme ( Waterhouse) ikiwa katika hatua za mwisho kukamilima kama inavyoonekana kwenye picha.

Akizungumza katika ziara hiyo Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa utekeleza wa mradi huo unaenda kasi na kwamba Kamati imeridhika na ujenzi wake ambao kwa sasa umefikia asilimia 74.
Sehemu ya mradi wa JNHPP ambapo maji yatatunzwa kwenda kuzalisha umeme ( Main Dam) ikiwa katika hatua za mwisho kukamilima kama inavyoonekana kwenye picha.

“Niseme sisi kama Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini tumeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huu mkubwa, kwani kufikia asilimia 74 za ujenzi ni jambo kubwa, kama mnavyoona hapa hizi transfoma zote 27 zikiwa ni moja ya miundombinu itakayo wekwa kwenye mradi huu wa JNHPP zinaashiria kuwa mradi upo mwishoni,"alisema Mhandisi Manyanya.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ikiangalia Transfoma zitakazotumika Katika mradi wa kuzalisha umeme wa JNHPP, mara baada ya kutembelea mradi huo Oktoba 15, 2022.

Aidha, Mhandisi Manyanya aliiomba serikali iwe na utaratibu wa kuwatambua vijana ambao wanatekelekeza miradi mikubwa ya kimkakati ili waweze kuendeleza ujuzi wao mahali ambapo wanatakiwa na katika utekelezaji wa miradi mingine nchini wapate kusaidia kwa ujuzi wao walioupata kutoka katika miradi hii mikubwa ikiwemo, JNHPP, Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR, Mradi wa ujenzi wa madaraja mbalimbali na meli ambapo kila mradi una vijana wanaopata ujuzi.

Mhandisi Manyanya alisema kuwa mradi huo umetoa ajira zipatazo 13,000 huku ajira 11,800 zikiwa ni kwa wazawa na ajira 1,200 zikiwa kwa Wageni na utagharimu fedha za kitanzania shilingi trilioni 6.5 na ukikamilika utaongeza megawatti za nishati ya umeme zipatazo 2,115 na kufanya kuwa na Megawatti 5,000 ifikapo mwaka 2025.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ikipata Maelezo kutoka kwa Watalaamu wa TANESCO waliopo Katika mradi wa kuzalisha umeme wa JNHPP, mara baada ya kutembelea mradi huo Oktoba 15, 2022.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania, Mhandisi Athanasius Nangali alisema kuwa wapo tayari kutekeleza mradi huo kwa ubora unaotakiwa ili uweze kusaidia kwenye uchumi wa nchi kama Serikali inavyoelekeza.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ikiwa katika eneo la kuzalishia umeme (Powerhouse) katika mradi wa kuzalisha umeme wa JNHPP, mara baada ya kutembelea eneo hilo Oktoba 15, 2022.

“Tutaendelea kufanya kazi usiku na mchana ili tu kuhakikisha kuwa mradi huu unakamalika kwa ufanisi mkubwa, kwa ubora unaotakiwa na wakati ili tuweze kuzalisha umeme wa kutosha kwa ajili ya kusaidia uchumi wan chi yetu”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news