NA MUNIR SHEMWETA, WANMM
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Khamis Hamza Chillo amewataka viongozi wa mikoa na wilaya nchini kutoa elimu ya upandaji miti kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Kamkolwe Kata ya Mpombwe Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Oktoba 11, 2022.(PICHA NA WIZARA YA ARDHI).
Aidha, ametaka viongozi hao kwenda kuelimisha wananchi namna bora ya kutunza vyanzo vya maji na kueleza kuwa changamoto kubwa iliyopo kwenye vyanzo hivyo ni shughuli kubwa za kibinadamu.
Amesema, maeneo mengi yanayovamiwa wavamizi wake hawaendi tu kuvamia bali wanakata na miti na kuharibu vyanzo vya maji ambapo aliwataka viongozi wa mikoa na wilaya kuwaeleza wananchi ambao vijiji vyao vitabaki basi wapande miti.
Akigeukia suala la utunzaji vyanzo vya maji, amesema mbali na uchafuzi wa mazingira unaofanywa wenye maeneo yaliyovamiwa, lakini wengine wanaharibu kabisa kwa kujenga nyumba na mwisho wa siku wanaharibu mazingira.
"Tusimsoneneshe rais kwa kuanzisha migogoro mingine maana atasikitika sana kwamba ametoa rasikimali fedha, watu na muda kumaliza migogoro halafu tuanzishe kamati nyingine na tujitahidi kuanzia ngazi ya chini ili kudhibiti migogoro inayoweza kutokea katika maeneo mengine,"amesema.
Ridhiwani Kikwete ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka watendaji wa sekta ya ardhi kuacha nidhamu ya woga kwa kutekeleza maelekezo ya wanasiasa bila kufuata taratibu.
"Wataalamu wetu waelekezeni viongozi wa siasa taratibu za kupata maeneo, mkituachia sisi tukioongoza harakati mwisho wa siku mnatengeneza hapa maeneo yote kuvamiwa na hakuna taratibu halafu mtakuja kusema walikuwa viongozi hawakufanya lolote kumbe wewe mwenyewe ni sehemu ya uvurugaji,"alisema Ridhiwani.
Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde aliwataka viongozi katika mikoa kuhakikisha kunakuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi hasa kupanga maeneo ya kilimo na wizara yake kwa sasa iko kwenye mchakato wa kutunga sheria ya kilimo ili kutunza maeneo yanayofaa kwa kilimo na kutumika kwa kazi hiyo.
"Tukiwapa maelekezo ya kutosha na kusimamia hatutafika hapa tulipofika na hii jamani tukitoka humu kila mtu akielewa tiyokubaliana akatekeleze,"amesema Masanja.