NA MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe.David Silinde (Mb) amesema Serikali imetoa agizo kwamba kwa Mikoa na Halmashauri zisisajili kijiji chochote au maeneo mapya ya utawala bila kushirikiana na Wizara nyingine za kisekta.


"Hatutasajili hayo maeneo mpaka kuwepo na ushauri au mapendekezo kutoka kwa Wizara za Kisekta kama Maliasili, Ardhi na nyinginezo," Mhe. Silinde amesisitiza.