NA MWANDISHI WETU
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bw.Kaspar Mmuya ametoa rai kwa watendaji wa Serikali kutunza vizuri vyombo vya usafiri walivyopewa ili viweze kuwasaidia katika utendaji wa kazi na kudumu kwa muda mrefu.

Wito huo umetolewa wakati wa kukabidhi bajaji mbili kwa watumishi wa Ofisi ya Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es Saalam katika kuwajengea mazingira mazuri watu wenye ulemavu ya utendaji wa kazi.

Akitoa neno la shukrani, Bw.Ophin Malley ameshukuru Serikali kwa kuwatambua watu wenye ulemavu katika mazingira waliyonayo mahala pa kazi.

“Tunaomba kama itafaa tuweze kupatiwa baiskeli maalumu ili zituwezeshe kuturahisishia kutoka sehemu moja kwenda nyingine wakati wa utendaji wa kazi,”amesema.