NA MWANDISHI WETU
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko katika kuisimamia Sekta ya Madini.

"Ndio maana mnaona nawagusa wote nawabadilisha,lakini Biteko yupo hapo katika Wizara ya Madini kwa sababu ninaye kijana anayefanya kazi nzuri na anaisaidia Tanzania," amesema Rais Samia.
Amesema, mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 4 na sasa unachangia karibu asilimia 8 ya mchango wake kwa Taifa.
Vile vile, amemtaka kuhakikisha mchango wa Sekta ya Madini unafikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025 ili iweze kuchangia zaidi katika Pato la Taifa.

Rais Samia amefanya ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Geita ambapo amezindua Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu kilichopo mkoani humo.