NA DIRAMAKINI
KATIBU Tawala Mkoa wa Geita, Profesa Godius Kahyarara ameshauri Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuanza kufikiria kuwekeza katika sekta ya madini kwa kuanzisha Migodi ya Dhahabu.
Ametoa ushauri huo Oktoba 5 ,2022 katika ukumbi wa kituo Cha uwekezaji (EPZ) katika Maonesho ya Dhahabu Mjini Geita wakati akifungua mafunzo maalum yaliyoandaliwa na NSSF kwa kushirikiana na Benki ya Azania pamoja Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO).
Aidha, Profesa Godius Kahyarara ameongeza kuwa hifadhi ya jamii ni zaidi ya kulipwa mafao ya uweezi kwani inasaidia hata katika uwekezaji na kujenga uchumi wa nchi.
Mafunzo hayo yaliyotolewa kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu wa pamoja na wasiliamali kutoka sekta binafsi ili kuwajulisha umuhimu wa kujiwekea akiba katika mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na na fursa za kuwawesha kupitia mfuko wa fursa kwa wote.
Akizungumza katika mafunzo hayo Meneja Sekta isiyo rasmi wa NSSF, Rehema Chuma amesema kuwa, kupitia Sheria ya Mifuko ya Jamii ya 2008 baada ya mabadiliko ya sheria hiyo mfuko huo umeruhusiwa kufikia kundi kubwa la wajasiriamali ambao hawako kwenye sekta rasmi.
Ameeleza kuwa, NSSF inafikia kundi la wachimbaji wadogo, wajasiriamali,ajira binafsi,limefikiwa ikiwa ni kundi kubwa kwenye uti wa mgongo wa taita.
Amewataka watu walioko kwenye makundi hayo kujiunga na NSSF ili waanze kuchangia kwa ajili ya usalama wao hasa kuwa uhakika wa pensheni ya uzeeni ambayo atalipwa hadi kufa kwake.
Meneja wa Benki ya Azani tawi la Geita, Rhoda Buluhya.
Amewataka wachimbaji wadogo kujiunga na mfuko huo ili kunufaika hasa pale wanapokuwa hawana nguvu za kuendelea kufanya kazi ngumu ya uchimbaji baada ya kuzeeka au uzalisha kupungua.
Vilevile amesema kuwa, kujiunga na NSSF kuna fursa ya kupata mikopo kupitia Benki ya Azania ambayo inatolewa kwa wanachama kwa lengo la kuchechemua uchumi pia.
Naye Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF,Bi.Lulu Mengele amesema kuwa, walikuwa na siku maalum kwenye maonesho ya tano ya teknolojia ya madini kwa ajili ya kuwafikia watu walioko kwenye sekta binafsi na isiyo rasmi.