Rais Dkt.Mwinyi awaapisha watendaji mbalimbali, waahidi kuchapa kazi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo amewaapisha watendaji mbalimbali wa Serikali kushika nyadhifa zao baada ya kuwateua hivi karibuni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo Valentina Andrew Katema baada ya kumuapisha kuwa Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar,kabla alikuwa Naibu Mrajis.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Valentina Andrew Katema kuwa Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar,kabla alikuwa Naibu Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi amemuapisha Mgeni Jeilani Jecha kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) pamoja na kumuapisha Valentine Andrew Katema kuwa Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar.Aidha, alimuapisha Shaheen Fauz Mohammed kuwa Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha Shahim Fauzi Mohamed kuwa Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. (Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo Shahim Fauzi Mohamed baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. (Picha na Ikulu).

Hafla hiyo ya kiapo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdalla, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said pamoja Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Mwinyi Talib Haji.
Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni miongoni mwa wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe,Zubeir Ali Maulid,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Haroun Ali Suleiman,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa leo.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara za Serikali, Viongozi wa Dini, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na wanafamilia.

Wakizungumza baada kiapo hicho, watendaji hao walimshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa kuwaamini na kuwateua kushika nyadhifa hizo na kuahidi kufanya kazi kwa juhudi na ushirikiano.

Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP), Mgeni Jeilani Jecha amesema ameazimia kuwahudumia wananachi wote kwa haki na usawa kwa kufuata Katiba ya Zanzibar na kuahidi kuweka mikakati maalum ya kukabiliana na wimbi la makosa ya jinai, hususani kesi za udhalilishaji wa kijinsia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimuapisha, Bw,Mgeni Jailani Jecha kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar baada ya kuteua hivi karibuni,kabla alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Uendeshaji na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo Mgeni Jailani Jecha baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar.

Amewataka wananchi kuwa na imani na Ofisi hiyo, huku akibainisha azma yake ya kuweka mikakati ya kuwashirikisha wananchi ili waweze kuwa na mwamko wa kufika mahakamani kutoa ushahidi.

Amesema atahakikisha anajenga ushirikiano wa karibu kati ya Ofisi ya DPP na wadau wengine wa masuala ya sheria ikiwemo Jeshi la Polisi, mahakama pamoja na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (ZAECA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news