NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Simba baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

“Kongole Simba kwa ushindi wa bao 1-0 (ushindi wa jumla 4-1) mlioupata dhidi ya Premiero De Agosto ya Angola na kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya Klabu Bingwa barani Afrika. Nawatakia kila la kheri katika michuano inayofuata.”
Ni kupitia mtanange uliopigwa leo Oktoba 16, 2022 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,.
Simba SC wameingia katika hatua hiyo kwa jumla ya mabao 4-1 kufuatia ushindi wa 3-1 waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Novemba 11 nchini Angola wiki iliyopita