Room to Read yawafikia watoto wa kike 6,000 katika elimu

NA ROTARY HAULE

SERIKALI Mkoani Pwani imeahidi kuendelea kushirikiana na Shirika la Room to Read linalojihusisha na utetezi wa haki za watoto wa kike hususani katika elimu kwa kuwa kazi wanayofanya inaleta matokeo chanya kwa Taifa.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani, Sara Mlaki ametoa kauli hiyo Oktoba 11 , 2022 katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani ambapo kwa upande wa Mkoa wa Pwani yalifanyika katika Halmashauri ya Mji Kibaha chini ya Shirika la Room to Read.

Mlaki amesema kuwa, kazi inayofanywa na Room to Read kwa kuwasaidia watoto wa kike katika elimu ndio jambo kubwa na muhimu kwa Taifa hili kwakuwa ndio lango la kuwainua watoto wa kike katika kutimiza ndoto zao.

Amesema kuwa,Room to Read wamekuwa msaada mkubwa nchini na mradi wanaoutekeleza ni wazi kuwa wanaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akipambana juu ya kusimamia haki za watoto wakike.
"Kipekee nitumie fursa hii kuwashukuru sana Room to Read kwa kuinua kiwango cha elimu kwa watoto wakike na hata kulinda haki zao na hii inaonyesha wazi kuwa Shirika hili linaungana na Rais Samia Suluhu Hassan katika kusimamia haki za watoto wakike kielimu,"amesema Mlaki

Mlaki ameongeza kuwa, Serikali pekee yake haiwezi kutekeleza mambo yote kwa wakati mmoja ndio maana inashirikiana na Room to Read pamoja na taasisi nyingine katika mapambano dhidi ya kutetea haki za watoto wakike.

Mlaki amepongeza juhudi za Room to Read katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa kike Duniani kwa kuwa wameuletea heshima Mkoa wa Pwani huku akiomba shirika hilo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kupiga vita vitendo viovu dhidi ya watoto hao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Room to Read, Juvenalius Kuruletera, amesema shirika hilo kwas asa limetimiza miaka 10 tangu lianze kufanyakazi ya kuwasaidia watoto wa kike hapa nchini.

Kuruletera amesema kuwa, mafanikio waliyoyapata katika kipindi chote hicho ni makubwa ikiwa ni kupunguza utoro ,mimba ,ndoa za utotoni,kuongezeka kwa ufaulu kwa watoto wakike, kuongezeka kwa uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike na hata kuwajengea uwezo wa kujiamini watoto hao.

Amesema,kuwa kupitia mafanikio hayo tayari mpaka sasa Shirika la Room to Read limewafikia watoto wa kike 6,000 na kwamba bado jitihada za kuwafikia watoto zaidi zinaendelea kwakuwa malengo ni kuhakikisha watoto wakike wanatimiza ndoto zao.
"Pamoja na mafanikio makubwa ambayo Room to Read tumeyapata lakini bado kuna changamoto zinazotukabili ikiwemo Serikali kuhitaji Shirika kuwafikia idadi kubwa ya wanufaika ili hali rasilimali chache,kutokuwepo kwa uelewa katika jamii kuhusu elimu kwa watoto wakike na hata uhitaji wa vifaa,"amesema Kuruletera.

Aidha, Kuruletera amemshukuru Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa elimu ndio maana ameweka mikakati mingi na kuwekeza katika elimu ili kusudi watoto wakike wapate elimu na kwamba lazima Shirika limuunge mkono.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mhandisi Mshamu Munde amepongeza juhudi za Room to Read hapa nchini na kusema Halmashauri yake imefanikiwa kupitia Shirika hilo.

Munde amesema kuwa, kwa sasa mambo yamebadilika kwa hiyo na tamaduni zinapaswa kubadilika kwa kuwa tamaduni za zamani zikifuatwa ni wazi kuwa zinawakandamiza watoto wa kike ambapo ameshauri kutumia tamaduni ambazo hazina kikwazo kwa watoto hao.
Hata hivyo,baadhi ya wanafunzi walioshiriki maadhimisho hayo akiwemo Shadia Mohammed wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari Bundikani na Spora Jeremiah kutoka Nyumbu Sekondari wamesema Shirika la Room to Read limewajengea ujasiri dhidi ya kujiepusha na vishawishi mbalimbali vya wanaume.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news