Serengeti Girls yafuzu kuingia robo fainali, Waziri Mchengerwa aipa kongole

NA JOHN MAPEPELE

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Soka ya Taifa wasichana U17 (Serengeti Girls) kwa kufuzu kuingia robo fainali baada ya kufungana bao 1-1 na Canada katika mechi iliyoisha hivi punde kwenye mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini India .
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mechi hii Mhe. Mchengerwa amesema wachezaji wameonesha uzalendo mkubwa kwa Taifa lao, na kusisitiza kuwa wanatakiwa kuendelea na uzalendo huo wa kucheza kufa na kupona ili kurejesha kombe nyumbani.

"Kwa niaba ya Serikali ninapenda kupongeza Sana timu yetu ya Serengeti Girls kwani wametambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kuiwakisha Tanzania katika mashindano haya" amefafanua Mhe Mohamed Mchengerwa.

Aidha, amesema ushindi huo umetokana na mchango mkubwa na msukumo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan anaoutoa katika Sekta za Michezo hapa nchini.

"Hapa ni lazima nimshukuru Mhe. Rais kwa maelekezo ya mahususi na kipaumbele anachotoa kwenye sekta hii," ameongeza Waziri Mchengerwa.
Kwa matokeo ya sasa Tanzania imefuzu Robo Fainali Kombe la Dunia la Wanawake chini ya Miaka 17 baada ya kuitoa Canada baada ya kupata sare ya Goli 1- 1 katika mechi ya Kundi D Uwanja wa DY Patil Mumbai.

Pia kwa matokeo haya, Tanzania Sasa inaungana na Japan katika hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo Kwa Kundi D.

Amewaomba watanzania kuiombea timu hiyo ili iweze kuendelea kushinda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news