NA HAPPINESS SHAYO-WMU
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema kuwa tathmini ya mipaka mipya ya Mapori ya Akiba yaliyopandishwa hadhi na kuonekana kuwa na changamoto ya muingiliano wa mipaka, haitagusa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu mipaka ya vijiji.



“Tathmini ilivofanyika ilibaini kuwa Hifadhi ya Msitu ya Mpanda Line, Tongwe West, Sehemu ya Hifadhi ya Msitu wa Masito, Eneo la Makazi ya Wakimbizi la Mishamo, Sehemu ya Maeneo ya Vijiji katika Kata ya Mishamo viliingizwa vyote kwenyePori la Akiba la Tongwe East lakini lengo ilikuwa ni kupandisha Pori la Akiba la Luganzo Tongwe.