NA MWANDISHI WETU
SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Ureno zimesaini Hati
ya Makubaliano ya kuanzisha Majadiliano ya Kisiasa baina yao ili
kuimarisha ushirikino kwa kuanzisha rasmi majadiliano ya kukuza
ushirikiano huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno, Mhe.Mhe. João Gomes Cravinho wakisaini Hati ya Makubaliano ya Kuanzisha Majailiano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Ureno. Hati hiyo imesainiwa hivi karibuni jijini Lisbon wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Dkt. Tax aliyoifanya nchini humo kuanzia tarehe 20 hadi 22 Oktoba 2022. Pamoja na mambo mengine kusainiwa kwa Hati hiyo kunatoa fursa kwa nchi hizi mbili kuanza majadiliano rasmi ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali ya manufaa kwa pande mbli kama vile biashara, uwekezaji, elimu na uchumi wa bluu.
Waheshimiwa Mawaziri wakibadilisha Hati hiyo muhimu mara baada ya kusaini.
Hati hiyo, imesainiwa
tarehe 21 Oktoba 2022 jijini Lisbon kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno, Mhe. João Gomes Cravinho.
Akizungumza
wakati wa mazungumzo rasmi kati yao, Mhe. Dkt. Tax amesema anaishukuru
Serikali ya Ureno na Serikali yake kwa hatua hii muhimu katika
ushirikiano wa kidiplomasia na kwamba kusainiwa kwa hati hiyo kunalenga
kuupeleka ushirikiano huo katika hatua nyingine ya juu ambapo nchi hizi
mbili zitaongeza zaidi ushirikiano katika maeneo mbalimbali yenye
maslahi kwao ikiwemo biashara, uwekezaji, utalii, uchumi wa buluu,
usafirishaji na elimu.
Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Gomes wakiwa katika mazungumza rasmi kuhusu namna ya kuimarisha na kuboresha ushirikiano kati ya Tanzania na Ureno.
Vilevile amesema kwamba hii ni
ishara kwamba nchi hizi mbili zina nia ya ya dhati ya kushirikiana
kwenye masuala mbalimbali ya manufaa kwa pande zote mbili.
“Ziara
yangu nchini Ureno imekuwa ni ya manufaa makubwa kwani kwa mara ya
kwanza katika historia ya ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hii
tumesaini Hati ya Makubaliano ya kuanzisha majadiliano ya kisiasa baina
yetu. Hii ni hatua ya juu katika ushirikiano wa kidiplomasia kwani sasa
masuala mengi ya ushirikiano kati yetu ikiwemo biashara, uwekezaji,
utalii, yataimarika na kwenda viwango vingine vya juu kwa manufaa ya
pande zote mbili,”alisema Dkt.Tax.
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakishiriki mazungumzo rasmi kati ya Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Gomes (hawapo pichani). Wa kwanza kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Ureno mwenye makazi nchini Ufaransa, Mhe. Samwel Shelukindo akifuatiwa na Brigedia Generali Mbaraka Mkeremy kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Bw. Charles Mbando, Katibu wa Waziri.
Mhe. Dkt. Tax (katikati) akimsikiliza Mhe. Gomes (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo rasmi kati yao. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambi ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme na kushoto ni Mhe. Balozi Shelukindo.
Ameongeza kusema kuwa,
wamekubaliana na Waziri mwenzake kuweka mikakati thabiti ya pamoja ya
ufuatiliaji wa utekelezaji wa maeneo mbalimbali ya ushirikiano
waliyokubaliana ambapo pia Mhe. Dkt. Tax amewataka Watanzania kutumia
hatua ya kusainiwa kwa mkataba huo kama chachu ya kuanza kuchangamkia
fursa mbalimbali zilizopo Ureno ikiwemo biashara kwa bidhaa za kahawa,
chai, samaki, viungo vya chakula na mbao.
Pia, wakati wa
mazungumzo yao, Tanzania imesisitiza umuhimu wa nchi hiyo kushirikiana
nayo katika medani za kimataifa hususan kuendelea kupaza sauti ili nchi
za Ulaya ziendelee kuisadia Tanzania na nchi za Afrika katika
kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya Tabianchi.
Maafisa kutoaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Gomes. Kushoto ni Bi. Liliani Kimaro na Bi. Sekela Mwambegele.
Kwa upande wake, Mhe. João Gomes
Cravinho amemshukuru Mhe. Dkt. Tax kwa kukubali mwaliko wake na
kutembelea nchini humo na kwamba Ureno inathamini mchango wa Tanzania
kupitia ushirikiano uliopo kati yao ikiwa ni pamoja na ushirikiano
katika medani za Kimataifa.
Amesema ana imani kuwa kusainiwa kwa
hati hiyo muhimu ni mwanzo mpya wa ushirikiano huo ambapo nchi hizi
mbili sasa zitazingatia na kujitoa zaidi katika kuhakikisha ushirikiano
uliopo unaimarika zaidi.
Mhe. Gomes akimkabidhi zawadi Mhe. Dkt. Tax mara baada ya kukamilisha mazungumzo rasmi.
“Hatua ya kusainiwa kwa Hati
hii ni ya kihistoria.. Kilichobaki sasa ni kuhakikisha yale
tuliyokubaliana leo na kupitia hati hiyo yanatekelezwa,” alisema Mhe.
Gomez.
Akizungumzia maeneo ambayo nchi hiyo imepiga hatua na ipo
tayari kushirikiana na Tanzania kuwa ni pamoja na eneo la Nishati
Mbadala.
Mhe. Dkt. Tax naye akimpatia zawadi Mhe. Gomes. Zawadi hiyo ni bidhaa za Tanzania ikiwemo Korosho, Kahawa, Asali, Batiki na Viungo vya Chakula.
“Hatua ya kusainiwa kwa Hati
hii ni ya kihistoria.. Kilichobaki sasa ni kuhakikisha yale
tuliyokubaliana leo na kupitia hati hiyo yanatekelezwa,” alisema Mhe.
Gomez.
Akizungumzia maeneo ambayo nchi hiyo imepiga hatua na ipo
tayari kushirikiana na Tanzania kuwa ni pamoja na eneo la Nishati
Mbadala.
Maafisa wanaosimamia masuala ya Sheria kutoka Tanzania na Ureno wakiandaa Hati ya Makubaliano kabla ya kusainiwa. Kushoto ni Bw. Ibrahim Mmbaga, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Alisema, nchi hiyo hadi sasa
imefikia asilimia 62 ya matumizi ya Nishati hiyo na kwamba malengo yao
ni kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2026.
Wakati wa mazungumzo
yao viongozi hao pia walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika masuala
ya biashara, elimu, utalii, sanaa na michezo pamoja na kukuza Lugha ya
Kiswahili kwa upande wa Ureno na Kireno kwa upande wa Tanzania.
Mhe. Dkt. Tax na mwenyeji wake Mhe. Gomes wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilisha mazungumzo kati yao.
Mhe. Dkt. Tax akiagana na Mhe. Gomes mara baada ya kukamilisha mazungumzo na kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano.
Picha ya pamoja.
Ziara ya Mhe. Waziri Tax nchini Ureno ni matokeo ya majadiliano kati ya Rais wa Ureno, Mhe. Rebelo De Sousa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Isdor Mpango walipokutana mwezi Juni 2022 pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari ambapo walizungumza kuhusu umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Mhe. Dkt. Tax amehitimisha ziara yake ya siku mbili aliyoifanya nchini humo kuanzia tarehe 20 hadi 22 Oktoba 2022 kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo,Mhe. João Gomes Cravinho. Itakumbukwa kuwa, Mhe. Waziri Tax alianza ziara yake nchini Poland kuanzia tarehe 17 hadi 19 Oktoba 2022 kabla ya kutembelea Ureno.