NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana ameihakikishia Serikali ya Ufalme wa Hispania kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na nchi hiyo katika kukuza na kuimarisha uhusiano uliopo kwa manufaa ya nchi na watu wake.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa na Balozi Mteule wa Ufalme wa Hispania nchini Mhe. Jorge Moragas Sánchez wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Taifa la Hispania iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt.Pindi Chana ametoa kauli hiyo katika hafla ya maadhimisho Siku ya Uhuru wa Taifa la Hispania iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Taifa la Hispania iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Ufalme wa Hispania katika kukuza na kuimarisha uhusiano wetu kwa maslahi mapana ya nchi zetu na wananchi,” alisema Mhe. Dkt. Pindi Chana.
Ameishukuru Hispania kwa kuendelea kuisaidia Tanzania kupitia sekta za maji, afya, umeme vijijini na kilimo na kuongeza kuwa ni matumaini yake kwamba ushirikiano huo utakuwa na kufikia sekta nyingine nyingi za kiuchumi.
Mhe.
Dkt. Pindi Chana pia ameishukuru Hispania kwa kuijumuisha Tanzania kuwa
moja ya nchi za Afrika zitakazonufaika na Sera Maalum ya Nchi za Afrika
iliyoanzishwa mwaka 2019.
Amesema
Hispania imekuwa mstari wa mbele katika maeneo ya afya, lishe, elimu,
mabadiliko ya tabia nchi na usawa wa kijinsia, maeneo ambayo ni ya
kipaumbele pia kwa Tanzania na kuongeza kuwa ni matumaini yake kwamba
Tanzania na Hispania zitaendelea kushirikiana katika maeneo hayo kwa
maslahi mapana ya nchi hizo.
“Kwa
miaka mingi Serikali ya Hispania imekuwa mstari wa mbele katika maeneo
ya afya, lishe, elimu, mabadiliko ya tabia nchi na usawa wa kijinsia,
hay ani maeneo ambayo Tanzania ni kipaumbele chake pia nina uhakika kuwa
Tanzania na Hispania zitaendelea kushirikiana katika maeneo hayo kwa
maslahi mapana ya nchi zetu” alisema.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa na Balozi Mteule wa Ufalme wa Hispania nchini Mhe. Jorge Moragas Sánchez wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Taifa la Hispania iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akiongelea kuhusu uhusiano wa kibiashara Dkt. Pindi Chana ametoa wito wa kuongezwa kwa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo na kuongeza kuwa ujazo wa biashara kati ya nchi hizo kwa mwaka 2021 ulikuwa sawa na Shilingi Bilioni 183.3.
Akiongelea Utalii,Dkt.Pindi Chana alisema watalii kutoka Hispania wamekuwa wakiitembelea Tanzania lakini watalii hao walipungua kutokana na janga la ugonjwa wa COVID 19 kutoka watalii 18,838 kwa mwaka 2019 hadi watalii 13,150 kwa mwaka 2021.
Alitoa wito kwa watalii wa Hispania kuja kwa wingi kuitembeleea Tanzania kutokana na kuwa na vivutio vya kipekee duniani na hawatasahau ujio wao hapa nchini.
Awali akimkaribisha Dkt. Chana katika hafla hiyo Balozi Mteule wa Ufalme wa Hispania nchini Mhe. Jorge Moragas Sánchez alisema Serikali yao ina nia ya kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuingiza maeneo mengi zaidi ya ushirikiano na kufanya kazi pamoja na kuiletea nchi maendeleo.
Alitaja mpango mradi wa upanuzi wa Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam ambao watakaoshirikiana na Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania kama mfano mmojawapo.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Taifa la Hispania iliyofanyika jijini Dar es Salaam wakijumuika.
“Tumekuwa na ushirikiano mzuri kati ya nchi zetu, tunataka kushirikiana zaidi katika maeneo ya Maendeleo, mfano ni kupitia mradi wa upanuzi wa Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam ambako tunashirikiana na Benki ya Dunia na Serikali kufanya kazi hiyo,” alisema.