NA DIRAMAKINI
MBUNGE wa Jimbo la Amani lililopo Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Mussa Hassan Mussa, amefariki dunia leo jijini Zanzibar.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson.
Aidha, Mheshimiwa Spika ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge pamoja na wananchi wa jimbo la Amani kufuatia msiba huo.
Kwa mujibu wa taarifa mwili wa marehemu unapelekwa kijijini kwao Bwejuu kwa ajili ya maziko yanatarajiwa kufanyika saa kumi leo baada ya sala ya alasiri.
Innalillahi waina ilaihi rajiun Allah amsameh makosa yake na awape subra wafiwa