Wamachinga:Polisi songeni mbele kudhibiti wahalifu nchini

NA DIRAMAKINI

SHIRIKISHO la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) limelipongeza na kulishukuru Jeshi la Polisi na uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuchukua hatua za haraka na kuweka taratibu na mbinu mbalimbali za kukabiliana na genge la vijana wahalifu maarufu Panya Road mkoani hapa.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam,Namoto Yusuph Namoto wakati akitoa tamko la SHIUMA Kuhusu mikakati inayoendelea ya jeshi la polisi kulitokomeza genge la Panya Road.

Pia Namoto amekemea baadhi ya wanajamii na baadhi ya wanasiasa ambao wanajaribu kubeza na kupotosha mchakato mzima unaoendelea wa kupambana na genge hilo la kihuni kitendo alichosema ni cha kupingwa kwa nguvu zote.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa Machinga Tanzania,Steven Lusinde ametumia nafasi hiyo kuwaasa vijana kutokufanya uhalifu kwa madai kuwa hakuna ajira na badala yake kujiunga na Umoja wa Machinga kwani ndani ya umoja huo kumekuwa na fursa za kutosha.

Nao baadhi ya wenyeviti wa machinga wilaya akiwemo Mwenyekiti Machinga Wilaya ya Ilala,Bakari Saidi Makupa na Mwenyekiti machinga wilaya ya Kigamboni Faida Nurdin Mohammed kwa pamoja wamepongeza kamati za ulinzi katika maeneo husika huku wakiwataka wazazi na walezi wa watoto ambao bado wanaojihusisha na vitendo hivyo kutoa taarifa ama kuwakemea ili waachane matukio hayo.

Hivi karibuni jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam liliendesha operesheni kamambe iliyofanikiwa kuwakamata vijana kadhaa wa genge hilo la panya road na baadhi yao kuuwawa

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news