Watanzania wang'ara zaidi duniani

NA JOHN MAPEPELE

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewapongeza washiriki wa Tanzania kwa kufanya vizuri na kutwaa ubingwa kwenye shindano la 12 la dunia la urembo, utanashati na mitindo kwa watu wenye matatizo ya usikivu.
Katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo Oktoba 30, 2022 Jijini Dar Es Salaam, Mrembo kutoka Tanzania Hadija Kanyama ameibuka mshindi wa taji la urembo la dunia huku Mtanzania Rajan Ally kuwa mshindi wa pili wa taji la utanashati wakati, Russo Songoro akishinda taji la wanaume upande wa mitindo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo, Waziri Mchengerwa amesema tamasha hilo ni miongoni mwa matamasha makubwa duniani ambalo limeiheshimisha Tanzania huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuamsha ari na kuinua vipaji vya watanzania na sasa vinaonekana na kuitangaza Tanzania dunia.

“Tunampongeza Mheshimiwa Rais, tunawapongeza watanzania wote kwa kuwa ushindi huu ni wa watanzania wote kwa ujumla na hii ndiyo tafsri ambayo Mhe. Rais amekuwa akitamani kuionyesha na kuwataka watanzania waionyeshe na kuonyesha vipaji vyao,"ameongeza Mhe.Mchengerwa.

Mshindi wa pili kwa upande wa Miss ni Chanika Vilioen kutoka Afrika Kusini wakati mshindi wa tatu ni Miseon Kang kutoka Korea kusini.

Kwa upande wa Mister, Mu-Australia Gareth Kelaart ametwaa taji hilo akifuatiwa na mtanzania Rajani Ally na nafasi ya tatu kuchukuliwa na Hung Nguyen kutoka Vietnam.

Upande wa Miss Deaf mwanamama Krista Trish Baggio kutoka Australia alitwaa taji hilo na Megan Holmes kutoka Afrika kusini kushika nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ikichukuliwa na Musuku Saritha kutoka India.

Katika upande wa vazi la kuogelea washindi watatu ni Ms Musuku Saritha kutoka India, Mr. Hillary Davido kutoka Uganda na Miss Keoleboge Khumoetsile kutoka Botswana.

Kundi la vipaji washindi watatu ni Miss Miseon Kang kutoka Korea Kusini, Mr Jean Mendy kutoka Senegal na Ms, Pamela Cuthel kutoka Australia wakati kwa upande wa vazi la utamaduni walioshinda ni Miss Lilian Opete kutoka kenya, Mr Gareth Kelaart kutoka Australia na Ms Megan Holmes kutoka Afrika Kusini.

Kwa upande wa mavazi ya muziki wa utamaduni walioshinda ni Miss Khadija Kanyama, Mr Marvelous Kundai Dziwire kutoka Zimbabwe na Ms Musuku Sarita kutoka India.

Kwa upande muonekano mzuri kwenye picha washindi ni Miss Josephine Kiden kutoka Sudan Kusini, Mr Hung Nguyen kutoka Vietnam na Ms Musuku SaritaKutoka India.

Na kwa upande wa mitindo kundi la wanawake ni Progress Madhibha kutoka Zimbabwe, wanaume Russo Songoro kutoka Tanzania na pande zote kutoka ni Exner Clemens kutoka Ujerumani.

Pia upande wa wabunifu wa mitindo ya mavazi Krista Trish Baggio kutoka Australia ameshinda kwa wanawake na wanaume ni Javed Latif kutoka India na kwa wote ni Mamadou Camara kutoka nchini Senegal.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news