NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe.Dkt.Selemani Jaffo tarehe 6 Oktoba, 2022 ameuagiz Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuweka vifaa maalum vya kutunzia taka katika maeneo mbalimbali nchini kwa namna ambavyo PSSSF watapendekeza ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya utunzaji wa mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Dkt.Selemani Jaffo (kushoto) akizungumza na Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea katika Banda la Mfuko huo katika Maonesho ya tano ya Sekta ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili EPZA Geita. (Picha na Hughes Dugilo).
Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jaffo (kushoto) alipofika kwenye Banda la Mfuko huo kujionea shughuli wanazozifanya katika Maonesho ya Madini Geita.
Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mfuko huo katika banda lao.
Pia Waziri Jaffo ameipongeza PSSSF kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulipa mafao kwa wakati na kuwawezesha wastaafu kuwa na uhakika wa maisha yao baada ya kustaafu.