Waziri Mkuu awasili Korea Kusini kwa ziara ya kiserikali

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Jumatatu, Oktoba 24, 2022 amewasili Seoul, Jamhuri ya Korea Kusini kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.

Mheshimiwa Majaliwa alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Togolani Mavura pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi katika nchi hiyo.

Kesho Jumanne, Oktoba 25, 2022 Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea kkampuni ya kutengeneza mabehewa na injini za treni cha SRT kilichopo katika mji wa viwanda wa Mungyeong pamoja na kituo cha ubunifu kilichopo Pangyo.

Aidha, akiwa Korea Kusini, Waziri Mkuu anatarajiwa kushiriki kongamano la biashara na kukutana na wamiliki wa makampuni makubwa na wenye viwanda. Vilevile, atakutana na Watanzania waishio Korea Kusini.

Kupitia vikao hivyo, Tanzania inatarajiwa kuimarisha mahusiano na Korea Kusini ambayo yamedumu kwa miaka 30. Vilevile, kukuza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji, kuangalia fursa za kukuza uchumi wa buluu, utalii, mahusiano ya anga na ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na utamaduni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news