NA MATHIAS CANAL
MBUNGE wa Jimbo la Rombo Mkoani Kilimanjaro ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe.Prof.Adolf Mkenda leo Oktoba 2,2022 ameongoza harambee ya ununuzi wa kiwanja cha Parokia ya Mtakatifu Pius X Tarakea Jimbo Katoliki Moshi.

Katika harambee hiyo kiasi cha shilingi milioni 82,841,900 kimepatikana ambapo ahadi ni shilingi milioni 36,313,000 na fedha taslimu zilizopatikaa ni shilingi milioni 46,528,900.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa harambee hiyo, Waziri Mkenda amewapongeza waumini wote kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kujitolea kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kanisa.

Prof.Mkenda amewahakikishia wananchi wa Rombo na waumini wa Parokia ya Mtakatifu Pius X Tarakea Jimbo Katoliki Moshi kuwa ofisi ya mbunge itaendeleza ushirikiano kwa ajili ya shughuli zote za maendeleo ya kanisa.

Kadhalika, Waziri Mkenda ametoa rai kwa kanisa kuendelea kushirikiana na Serikali kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wote.