NA MWANDISHI WETU
IMEELEZA kuwa jumla ya Asasi za Kiraia (AZAKI) 500 zinakusudiwa kuhudhuria katika Wiki ya AZAKI iliyopangwa kufanyika kwa siku tano kuanzia Oktoba 24 hadi 28 katika Ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC) jijini Arusha.

Aidha ameongeza kuwa Wiki ya AZAKi inaelekeza juhudi zake katika kuhakikisha ushirikishwaji bora wa watendaji kutoka sekta mbalimbali hapa nchini.
“Kongamano hili litafanyika mkoani Arusha kwa muda wa siku tano na litakuwa la tofauti na miaka iliyopita kwa sababu tutakuwa na washiriki kutoka katika makundi tofauti, wapo washiriki ambao wametoka katika mashirika ya ndani na mashirika ya kimataifa na ushiriki mkubwa sana kutoka mashirika binafsi.
”Wiki hii inawaleta pamoja wadau wakuu wa maendeleo na inalenga kuimarisha mahusiano na ushirikiano unaolenga kuimarisha ushiriki wa asasi za kiraia katika maendeleo ya Tanzania, kuunda jumuiya mpya na kuimarisha jumuiya zilizopo zenye lengo la kutatua changamoto kuu za maendeleo na kubadilishana mawazo,”amesema Kiwanga.
Kiwanga ameongeza kuwa asasi za kiraia znafanya kazi kwa karibu na watu na jamii kwa ujumla kupitia utekelezaji wa afua zinazosaidia uendelezaji wa usawa wa kijinsia, ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu, demokrasia, ushiriki wa vijana, amani na mshikamano wa kijamii.
‘’Sekta ya asasi za kiraia iinnaendelea kutumia mbinu bunifu ili kuchochea maendeleo ya watu. Tuna nia ya kuwa na mijadala inayozingatia watu. Kama sekta ya mashirika ya kiraia, tunaelewa kwamba tunaweza tu kutekeleza masuluhisho ya kimaendeleo kwa sauti za watu. Ushiriki wa watu katika maendeleo yao na kuwa na sauti juu ya changamoto zao ambazo ni muhimu zikapatiwa utatuzi,"ameongeza.
Katika hatua nyingine Kiwanga amezungumzia suala la mabadiliko ya tabia nchi ambapo amesema upo uwezekano wa kuwepo na uhaba wa chakula kutokana na uhaba wa uzalishaji wa mazoea.

“Kikao chetu kinalenga kujadili athari za mikopo inayotolewa na Serikali katika maisha ya watu na maeneo yanayopendekezwa kuboreshwa. Pia Kikao hicho kitahusisha kutoa shuhuda kutoka kwa wajasiriamali waliofanikiwa,’’amesema.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Sekta ya Umma Benki ya Stanbic, Doreen Dominic amesema kuwa kama Sekta Binafsi wanalojukumu kubwa la kuwanyanyua wananchi katika shughuli za kiuchumi kwa kuwawezesha katika kazi zao za uzalishajimali zikiwemo Biashara.
Amesema, kwa sasa benki hiyo inatambua kuwepo kwa juhudi kubwa zinazofanywa na wadau wa maendeleo na kwamba watahakikisha wanaunga mkono juhudi hizo ili kuendelea kuisaidia jamii ya watanzania.
“Tunatambua kuwa Kuna uwekezaji mkubwa nchini Sasa tunahitaji kuwanyanyua wananchini wakiwemo wafanyabiashara kwenda juu ili kuweza kupata fursa zinazotokea katika nchi yetu kwa Sasa,"amesema Doreen.