NA DIRAMAKINI
UJIO wa Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan mkoani Manyara umepokelewa kwa kishindo na vijana wa boda boda ambao waliamua kufanya maandamano makubwa ya kumpokea Kiongozi huyo wa Kitaifa.

Aidha, bodaboda hao pia wameishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kuwa mikopo ya asilimia nne, kupitia Halmashauri ya Babati.