NA DIRAMAKINI
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeufungulia Uwanja wa Jamhuri uliopo mkoani Dodoma kuendelea kutumika kwa michezo ya ligi baada ya kukaguliwa na kuthibitishwa na Kamati ya Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) ya Leseni za Klabu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 27, 2022 na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uwanja huo umefanyiwa maboresho katika maeneo yote muhimu likiwemo eneo la kuchezea (pitch), vyumba vya kuvalia na uzio unaotenganisha mashabiki na eneo la kuchezea.
"Kwa mujibu wa Kanuni ya 9:8 ya Ligi Kuu, uwanja huo utaruhusiwa kwa michezo ya ligi kuanzia Desemba 10, 2022 ikiwa ni siku 14 tangu ulipokaguliwa na Kamati ya TFF ya Leseni za Klabu, Novemba 26, 2022,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.
Pia Bodi ya Ligi imeendelea kuzikumbusha klabu kuhakikisha viwanja vyao vya nyumbani vinakuwa katika hali ya ubora wakati wote ili vikidhi matakwa ya kanuni na sheria za mpira wa miguu.

Tags
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania
Habari
Ligi Kuu Tanzania Bara
Ligi Kuu ya NBC
Michezo
Uwanja wa Jamhuri Dodoma