NA DIRAMAKINI
KATIKA kuhakikisha wanaboresha na kusogeza huduma zake karibu zaidi kwa wateja wao China Dasheng Bank Ltd imezindua tawi jipya katika mtaa wa Agrey na Lumumba Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi Mkurugenzi wa benki hiyo,Jimmy Mrosso amesema Benki ya China Dasheng ni benki inayokua kwa haraka na yenye mtaji wa kutosha.
Mrosso amesema, kwa sasa benki hiyo inapatikana nchini ambapo uzinduzi wa tawi hilo ni wa pili na hivyo matarajio yao ni kuendelea kufungua matawi nchi nzima ili kusogeza huduma karibu zaidi kwa wateja wake.
“Lengo kubwa la kuanzishwa kwa benki nchini ni kuataka kuunganisha uchumi wa Tanzania na China moja kwa moja, hatuwezi kupuuza umuhimu wa uchumi wa China kwa Tanzania,"amesema Mrosso.
Amesema, benki hiyo ambayo imekuwa kwa kasi nchini imeanzishwa rasmi kwa malengo la kuunganisha uchumi wa Tanzania na China moja kwa moja.
Mrosso ameongeza kuwa, benki hiyo inategemea kuwekeza zaidi ili kuongeza zaidi faida kwa wateja wao na kwa faida ya Tanzania na China kwa ujumla.
"Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha watanzania kujiunga na benki hii kwa lengo la kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwepo kwa benki hii nchini kuwanufaika kiuchumi,"amesema Bw. Mroso.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo Poniwoa Mbisse amesema, wanayo furaha kufikisha miaka minne nchini ya kutoa huduma tangu ilipoanzishwa.
Aidha, Mbisse amechukua nafasi hiyo kuwashukuru Watanzania kwa kufanikisha mafanikio yao kwani bila wao wasingefikia hapo walipo.
"Leo tunatimiza miaka minne tangu kuanza kutoa huduma zetu nchini Tanzania napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru watanzania wote kwa jinsi walivyoipokea benki yetu kufikila malengo ya benki ya kuongeza mahusiano kati ya Tanzania na China,"amesema.