China yasamehe baadhi ya madeni ya Tanzania

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa Mikataba na Hati za Makubaliano ya kimkakati 15 akiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping.

Miongoni mwa mikataba hiyo iliyolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji wa baina ya nchi hizo mbili umeshuhudia China ikiipunguzia Tanzania sehemu ya deni lake la thamani ya Shilingi Bilioni 31.4.

Miongoni mwa mikataba na makubaliano yaliotiwa saini ni kuhusu mahitaji ya kuwepo na soko kubwa la usafirishaji wa maparachichi kutoka Tanzania kwenda China.

Pia wametia saini Mkataba unaohusu msaada wa RMB milioni 100 za ushirikiano wa kiuchumi na kitaalamu baina ya nchi hizo mbili.

Vile vile, kumetiwa saini makubaliano kuhusu mahitaji ya kuwepo na soko kubwa la Usafirishaji wa Mabondo ya Samaki pamoja na bidhaa nyingine za uvuvi kutoka Tanzania kwenda China.

Aidha, China imetoa mkopo wa thamani ya dola za Kimarekani milioni 56.72 wenye masharti nafuu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar, Terminal II.

China inaongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania. Hadi kufikia Mwezi Oktoba 2022, Jumla ya miradi 1,098 yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 9.6 ilisajiliwa katika kituo cha uwekezaji cha TIC.

Miradi hiyo imezalisha ajira 131,718. Uwekezaji huo umefanyika katika sekta za viwanda, kilimo, mawasiliano, madini na uvuvi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping wakishuhudia wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news