NA JOHN MAPEPELE
TAMASHA la Kimataifa la 41 la Utamaduni na Sanaa Bagamoyo linaanza leo Novemba 10, 2022 mjini Bagamoyo mkoani Pwani kwa kufanya kongamano itakalojadili kwa kina masuala ya sanaa na uchumi litalaloongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa.



Kesho, ambayo ni siku ya pili ya Tamasha, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt, Philipo Mpango atafungua rasmi tamasha hilo ambapo usiku vikundi mbalimbali vitatumbuiza na Mgeni maalum katika usiku huo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Siku ya mwisho, tamasha litatamatishwa na burudani kali kutoka kwa wasanii mbimbali ambapo Mgeni maalum atakuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul.