'IMARISHENI USIMAMIZI MFUMO WA GoT-HoMIS'

NA MWANDISHI WETU

UONGOZI wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imetakiwa kuimarisha usimamizi katika mfumo wa ukusanyaji mapato GoT-HoMIS ili kudhibiti upotevu wa fedha na kuboresha utoaji wa huduma za Afya katika hospitali hiyo.
Wito huo umetolewa na timu ya usimamizi shirikishi kutoka Idara ya Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Novemba 24,2022 baada ya kubaini kuwa bado kuna changamoto katika ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo wa GoT-HoMIS kitendo ambacho kinapelekea upotevu wa mapato.
Akiongea kwa niaba ya timu ya usimamizi shirikishi, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Ntuli Kapologwe ametoa wito kwa uongozi huo kushughulikia changamoto zilizopo ikiwemo changamoto ya ukosefu wa kompyuta.
"Ukususanyaji wa mapato hapa unasuasua tuna mfumo wa GoT-HoMIS kwanini tusiwekeze nguvu huko, mfumo huu ni mzuri sana katika kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha,"amesisitiza Dkt. Kapologwe.

Kwa upande mwingine timu ya usimamizi shirikishi kutoka OR-TAMISEMI imempongeza mganga mfawidhi wa kituo cha afya Natta kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na kupelekea makusanyo ya kituo hiko kupanda kutoka Shilingi laki nne hadi kufikia Shilingi milioni tatu kwa mwezi.
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Natta Dkt. Juma Kipingu amesema kuwa ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo wa GoT-HoMIS imesaidia kudhibiti upotevu wa mapato ambayo yametumika katika kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya,kulipa stahiki za watumishi pamoja na kukarabati majengo ya kituo hiko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news