Mary Daniel aibuka kidedea Mwenyekiti UVCCM mkoani Mara

NA FRESHA KINASA

DADA Mary Daniel ameshinda nafasi ya Uwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mara kwa kupata kura 369 na kumshinda mpinzani wake,Baraka Richard aliyepata kura 207 kati ya wajumbe 577 waliopiga kura huku kura moja ikiharibika.
Aidha, uchaguzi wa nafasi hiyo ulirudiwa mara ya pili kwa mujibu wa kanuni toleo la mwaka 2017 ibara ya 21 (b) kutokana na kukosekana mshindi kati ya wagombea hao watatu aliyekuwa amepigiwa kura na kuvuka asilimia 50 na ndipo wagombea wawili kati ya watatu wa nafasi hiyo waliokuwa katika mchuano mkali kupigiwa kura.

Nafasi ya Uwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara ilikuwa ikiwaniwa na Baraka Richard, Mary Daniel pamoja na James Matiko Ibanda ambaye katika marudio ya mara ya pili hakuweza kupigiwa kura kwa mujibu wa kanuni.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Novatus Kibaji amesema kwamba, baada ya uchaguzi huo kurudiwa awamu ya pili mgombea Baraka Richard aliweza kutoa malalamiko ikiwemo kudai kuna watu wamekamatwa na rushwa pamoja na kuona mtu akitembea nje kwa kigezo cha kushawishi wapiga kura jambo ambalo msimamizi huyo amesema madai hayo hayana mashiko.

"Awamu ya kwanza wagombea wote walisema mchakato wa uchaguzi umeenda vizuri kila hatua, lakini baada ya kurudia mgombea Baraka Richard alitoa malalamiko hayo na Mimi nahusika na usimamizi wa uchaguzi wa ndani hayo ya nje sina uhakika nayo na madai kwamba kuna watu wamekamatwa na rushwa Mimi sijawaona. Ninaamini uchaguzi huu umefanyika kwa haki kabisa na pia kama kuna malalamiko anayo zipo taratibu za kufuatwa, Mimi kama Msimamizi wa uchaguzi namtangaza Mary Daniel kuwa mshindi halali wa nafasi ya uwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara,"amesema Novatus.

Pia matokeo mengine ni nafasi ya Mkutano Mkuu UVCCM Mkoa ambapo wapiga kura walikuwa 556 kura moja imeharibika na Tabitha Amos amepata kura 277, Bhoke Wakuru kura 154 na Tubesti Noel kura 124.

Nafasi ya Mwakilishi wa UVCCM kwenda UWT kura zilizopigwa ni 536, kura zilizoharika ni mbili, kura halali 534 ambapo Cecilia Sobera amepata kura 270, Janeth Samwelly kura 153, na Bhoke Wakuru kura 111.

Nafasi ya Mwakilishi kutoka UVCCM Mkoa kwenda Wazazi wapiga kura walikuwa 512, kura 1 imeharibika na kura halali ni 511, ambapo Gacha beda amepata kura 39, Matambo Mazaga kura 91, na Tabitha Amos kura 381.

Nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa wapiga kura walikuwa 527, kura zilizoharika 5, kura halali 522 ambapo Janeth Samwelly amepata kura 261, Geoffrey Kasonyi kura 194, na Juliana Selemani kura 67.

Nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM Taifa wapiga kura walikuwa 529, kura iliyoharibika 1, na kura halali 528 ambapo Kamara Japhet alipata kura 137, Beatrice Mseti kura 187, na Christopher Cosmas kura 204 na baada ya matokeo kurudiwa kutokana na mshindi kushindwa kupata zaidi ya asilimia 50 uchaguzi ulirudiwa upya na wapiga kura walikuwa 482, kura iliyoharika ni moja, na kura halali 481, ambapo Beatrice Mseti amepata kura 286 na Christopher Cosmas kura 195.

Nafasi ya Mjumbe wa baraza kuu kura zilizopigwa zilikuwa 574, kura moja iliharibika, na kura halali 573, ambapo Machage Mwema amepata kura 103, Derfin Mayamba 210 na Paul Mwikwabe kura 260 na hakuna aliyevuka nusu hivyo uchaguzi ulirudiwa na wapiga kura walikuwa 562,na hakuna kura iliyoharika Deefin Mayamba amepata kura 232, na Paul Mwikwabe kura 330.

Na nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa, Paul Mwikwabe amepata kura 330 na hivyo atawakilisha nafasi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news