MHE.MASANJA:KUCHUNGA MIFUGO KATIKA MAENEO YA HIFADHI NI KUVUNJA SHERIA

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imekemea vitendo vya baadhi ya wananchi wanaochunga mifugo na kufanya shughuli za kilimo kwenye maeneo ya hifadhi za misitu ikieleza kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha Sheria ya Misitu Sura ya 323 inayokataza kuingiza au kuchunga mifugo kwenye maeneo ya yaliyohifadhiwa.
Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja(Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Kusini , Mhe. Innocent Kalogeris aliyetaka kujua ni lini Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) itaanza kutoa vibali vya malisho kwa wafugaji kama inavyotoa vibali vya kuvuna mbao na mkaa na kuwezesha Serikali kupata mapato.

“Ni dhahiri kuwa kuchunga, kulisha mifugo au kufanya shughuli za kilimo kwenye maeneo ya hifadhi za misitu ni kuvunja sheria, Serikali imeyahifadhi maeneo ya misitu kwa lengo la kulinda rasilimali zilizomo kwa matumizi endelevu ya kizazi cha sasa na kijacho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news