Mheshimiwa Sagini atoa rai kwa Jeshi la Uhamiaji

NA DIRAMAKINI

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Jumanne Sagini, amelitaka Jeshi la Uhamiaji nchini kutimiza wajibu wao kikamilifu kwa kufanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria za nchi ili kuwa na ufanisi.
Ameyasema hayo Novemba 29, 2022 wakati akifungua mafunzo ya kikao kazi mkoani Kilimanjaro yanayofanyika kwa siku mbili mkoani humo ambapo mafunzo hayo yanawahusisha viongozi wa ngazi zote kutoka Idara ya Uhamiaji.
Pia, Mheshimiwa Naibu Waziri Sagini amekabidhi magari mawili kwa Wilaya ya Rombo na Same yaliyonunuliwa na kamati ya usalama barabarani kwa ajili ya kusaidia kuimarisha doria hasa katika barabara ya Same ili kuimarisha usalama na amani.
Naibu Waziri Sagini pia, amewapongeza wananchi wa Kata ya Mwika Kaskazini mkoani Kilimanjaro kwa ujenzi wa Kituo cha Polisi kilicholidhi vigezo ambacho kitasaidia kuimarisha hali ya usalama na amani kwa wananchi na kuwawezesha kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo kwa ufanisi.
Katika hatua ngingine, Naibu Waziri Sagini ametoa rai kwa wakazi wa Kata ya Mwika Kaskazini wilayani Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro kuachana na matumizi ya pombe kali hasa kwa vijana.
Mheshimiwa Sagini amesema, wananchi hao waachane na matumizi ya pombe hizo kali na kwamba, vijana ni nguvu kazi na ni tegemeo kwa taifa ikiwemo kuchangia maendeleo na uzalishaji. Hivyo matumizi ya pombe kali kwa vijana inachangia kupoteza nguvu kazi ya ujenzi wa taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news