MTIHANI MWEMA:Wasomeeni wanafunzi huu ujumbe kabla hawajaingia kwenye mtihani

NA DR.MOHAMED OMARY MAGUO

LEO Novemba 14, 2022 jumla ya watahiniwa 566,840 wanatarajiwa kuanza kufanya mtihani wa kidato cha nne katika shule za Tanzania Bara na Zanzibar.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Athumani Amasi ameyasema hayo Novemba 13, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema, mtihani huo utafanyika katika jumla ya shule 5,212 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 1,794 nchini kote

Mtunzi na mshairi wa kisasa ambaye pia ni Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dkt. Mohamed Omary Maguo ameandaa utenzi mfupi wa kuwatakia mtihani mwema wanafunzi wa kidato cha nne wanaoanza mitihani yao leo nchini kote Tanzania.

Pia anawaomba walimu wawasomee wahitimu kwenye parade asubuhi kabla hawajaingia kwenye mtihani, endelea;


1:Kheir nyingi Baraka
-Form_ _four_ ziwafika
Mtulie pasi shaka
Mtihani ta'faulu

2:Mtihani ukiushika
Usome ukasomeka
Sijeanza tetemeka
_Material_ _ta'evaporate_

3:Kwa uwezo wa Malika
Lo'soma ta'yakukumbuka
Siogope paparika
Sheria ukazibananga

4:Kwa uwezo wa Rabuka
Fikra zitafunguka
Maswali yote kujibika
Kwa weledi na sahihi

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news