Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuendesha Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Amani Mkoa wa Mjini Magharibi Tanzania Zanzibar na Udiwani katika Kata 12 za Tanzania Bara tarehe 17 Desemba, 2022.
Uchaguzi Mdogo utafanyika katika Kata 12 za Tanzania Bara ambazo ni:-
Kwa mujibu wa kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ina jukumu la kutoa Elimu ya Mpiga Kura nchi nzima, kuratibu na kusimamia watu wanaotoa elimu hiyo. Elimu hiyo hutolewa ili kuwawezesha wapiga kura na wadau wa uchaguzi kushiriki vyema kwenye mchakato wa uchaguzi.
Kupitia tangazo hili, Tume inakaribisha taasisi na asasi zenye nia ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura katika Uchaguzi Mdogo kuwasilisha maombi yao. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 09 Novemba, 2022.
Taasisi/asasi itakayowasilisha maombi inatakiwa kukidhi vigezo vifuatavyo:-
1) Iwe na usajili kwa mujibu wa Sheria za Tanzania;
2) Iwe imefanya kazi Tanzania si chini ya miezi 6 toka kusajiliwa kwake;
3) Miongoni mwa watendaji wake watatu, wawili wanapaswa wawe watanzania;
4) Iwe haina taarifa za kuvuruga amani au kuchochea fujo ndani ya Jamhuri ya
Muungano na katika nchi yeyote; na
5) Iwe tayari kujigharamia katika kutoa Elimu ya Mpiga Kura.
Aidha, maombi hayo yanatakiwa kuambatishwa na:-
Aidha, maombi hayo yanatakiwa kuambatishwa na:-
1) Cheti cha Usajili;
2) Katiba ya Taasisi/asasi;
3) Majina ya viongozi wa juu wa taasisi/asasi
4) Anuani kamili ya makazi na namba za simu za ofisi na viongozi; na
5) Ratiba ya maeneo ambayo taasisi/asasi inatarajia kutoa elimu ya mpiga kura.
Tume haitahusika na utoaji wa rasilimali fedha za kugharamia zoezi la utoaji wa
Elimu ya Mpiga Kura kwa asasi zitakazopewa kibali.
Maombi yote yatumwe kwa anuani zifuatazo:-