NEC yateua madiwani 10 viti maalum Bara

NA GODFREY NNKO

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanya uteuzi wa wa madiwani wanawake wa viti maalum 10 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika halmashauri 10 za Tanzania Bara.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba Mosi, 2022 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera Charles.

"Katika kikao cha Oktoba 29, 2022 Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia kifungu cha 86A(1) ya Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na kifungu cha 35 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (mamlaka za wilaya) Sura ya 288, imewateua madiwani wanawake wa viti maalum 10 kujaza nafasi za madiwani katika halmashauri 10 za Tanzania Bara,"amefafanua Dkt.Charles.

Aidha, amebainisha kwamba, uteuzi huo unafanyika baada ya tume kupokea barua kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, yenye Kumb.Na. CCB.126/443/01 ya Septemba 12, 2022.

Dkt.Charles amefafanua kuwa, barua ya Waziri iliiarifu tume kuhusu uwepo wa nafasi wazi za madiwani wanawake wa viti maalum katika halmashauri 10 za Tanzania Bara zilizotokana na vifo.

Walioteuliwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na halmashauri zao katika mabano ni Lidia Msongele (Mbeya), Mariam Makasi (Mpwapwa), Bahati Shaban (Nzega).

Pia kuna Sauda Irumba (Kaliua), Theresia Mlay (Moshi), Monica Madiwa (Handeni), Hajida Ngope (Tandahimba), Hapines Kingu (Iramba), Zainabu Mabrouck (Kongwa) na Zainabu Orty (Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news