NA URBAN EPIMARK
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda anatarajia kutunuku vyeti wahitimu 80 wa kozi ya Uandishi wa Habari za Biashara iliyotolewa na Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Taasisi ya Bloomberg Media Initive Afrika (BMIA) ya kutoka nchini Marekani siku ya Jumatano Novemba 16, 2022.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda.
Tukio hilo litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Kibo Ballroom wa Hyatt Reagency Hotel (The Kilimanjaro) ya jijini Dar es Salaam, litahudhuriwa pia na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Prof Florens Luoga pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof William Anangisye.
Taarifa iliyo tolewa jijini Dar es Salaam na Mratibu wa shughuli hiyo anae tokea Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (School of Journalism & Mass Communication) Dr Zakaria Malima imeeleza kwamba, wahitimu wote 80 wanatakiwa kuwa tayari eneo la ukumbi huo saa moja unusu asubuhi ili kuanza mazoezi ya mahafali kabla ya Mgeni rasmi kuwasili kunako saa Nne kamili asubuhi.
Baadhi ya wakufunzi wa kozi ya Bloomberg Media Initive Afrika (BMIA) kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa kozi hiyo katika eneo la bustani ya Hoteli ya Hyatt Reagency (The Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam mnamo mwezi Februari 2020.
Mmoja ya wahitimu wa kozi hiyo Bw Beatusi Bihigi ambae ni Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Geita (Geita Press Club-GPC) ambae tayari yupo jijini Dar es Salaam amesema ni heshima kubwa kwake kuwa mmoja wa wahitimu hao hapa nchini, hivyo anategemea taaluma aliyoisomea na kuhitimu, itakuwa ya manufaa makubwa kwake.
Taasisi hiyo ya Bloomberg Media Initiative Afrika, iliendesha na kudhamini mafunzo hayo ya hadhi ya juu ya kimataifa ya jinsi ya kuripoti kwa ufasaha taarifa za fedha na biashara katika uandishi wa habari za biashara yaliyofanyika hapa nchini mwaka 2019 kwa awamu ya kwanza na kisha kufanyika tena baadae awanu ya pili.
Baadhi ya wahitimu katika kozi ya Bloomberg Media Initive Afrika (BMIA) wakiwa katika picha ya pamoja kwenye bustani ya Hyatt Regency Hotel (The Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam mwezi Februari 2020.
Mafunzo hayo yanalenga kuongeza tija zaidi katika kuchambua na kuripoti thamani ya matumizi ya fedha zinazo wekwa kwenye miradi mikubwa yenye manufaa mapana zaidi kwa jamii ili kuelezea thamani halisi uwekezaji huo.
Picha ya pamoja ya wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wahitimu wa kozi ya Bloomberg Media Initive Afrika (BMIA) awamu ya kwanza iliyofanyika hapa nchini wakiwa mbele ya bustani ya Hyatt Regency Hotel (The Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mafunzo yao mnamo mwezi Februari 2020.