*Mapendekezo yangu ni haya, ukuaji ili uende kasi ndugu zangu lazima tuwe na bidhaa nyingi mpya katika soko sio kuongeza tozo
*Tozo na kodi hazikuzi uchumi, kinachokuza uchumi ni bidhaa kwenda kwenye soko la ndani na nje, hivyo mipango yetu na bajeti lazima itueleze hivyo
*Mapendekezo yangu ni wataalam twende kwenye kilimo kina asilimia 30 ya GDP yetu hebu tupigane tufikie asilimia 40 sasa sitaki kurudia haya, haya nilishayaongea mazao ambayo lazima tuyawekee mkazo ni yale ambayo tunatumia ndani na nje ya nchi
NA FRESHA KINASA
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza kujadili Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Mwongozo wa kuandaa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2023/2024.
Katika majadiliano hayo Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara,Prof.Sospeter Muhongo leo Novemba 8, 2022 bungeni jijini Dodoma ameshiriki kikamilifu kutoa maoni na mapendekezo yake.
DIRAMAKINI kupitia mwandishi wake mwandamizi Kanda ya Ziwa, Fresha Kinasa inakusogezea alichokisema Prof.Muhongo hatua kwa hatua, endelea;
"Katika mjadala wetu tunaofanya sasa nadhani tutakuwa tumejifunza bajeti tunayoitayarisha mambo yaliyotokea MV Bukoba na yaliyotokea juzi tutayaona kwenye mpango na bajeti ya mwaka unaokuja.
"Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mjadala wetu lazima tujue malengo yake, mipango tunayoifanya iko ndani ya miaka mitano ambayo inaisha 2025 ambayo malengo yake ni ukuaji wa uchumi. Upatikanaji wa ajira mpya, huduma bora kwa wananchi na ndio maana vyote hivi Mheshimiwa Mwenyekiti hatuwezi kukwepa.
"Pendekezo ambalo tumelitoa mara kwa mara lazima tuwe na Planning Commission ambayo iko ndani ya Ofisi ya Rais. Sasa malengo ya kwetu Mwenyekiti ambayo yako kwenye hii document inasema kwamba ikifika mwaka 2025 tunataka GDP per capital yetu iwe dola 3,000.
"Hiyo inamaanisha kwamba, ikiwa sasa hivi tuko watu tunakaribia milioni 62 kufika 2025 huenda tunaweza kuwa watu milioni 68 tukafika milioni 70 maana yake ni kwamba. Ukichukua GDP per Capital dola 3,000 kwa kila mtu kwa mwaka tukifika mwaka 2025 tunapaswa kuwa na GDP isiyopungua dola Bilioni 200.
"Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi GDP yetu ni Dola bilioni 62 kwa hiyo huu mpango na bajeti yake ni lazima utuweke kwenye barabara kutoka Dola Bilioni 62 sasa kwenda Bilioni 200. Ni kazi kubwa kweli kweli na hapa lazima mipango yetu tuelezane ukweli tuone kama hilo lengo la GDP ya dola 3000 per Capital lilikuwa sahihi ama tuliandika tu kwa haraka haraka,"Mheshimiwa Prof.Muhongo amebainisha.
Mbunge huyo wa Musoma Vijijini ameendelea kufafanua kuwa, "Kwa sasa hivi, sisi tukiwa na Bilioni 62 GDP per Capital yetu inakadiriwa mwishoni mwa mwaka itakuwa GDP per Capital itakuwa 990. Kwa maneno mengine tunarudi chini, tunarudi kwenye group la nchi maskini. Kufiatana na viwango vilivyowekwa na Benki ya Dunia tarehe 1/7 mwaka jana, kwa hiyo tumeshuka. Tusiongelee uchumi wa Kati hatuko huko tena, tumeshuka.
"Wakati huo huo sisi tukiwa hivyo, wenzetu wa Kenya ikifika mwishoni mwa mwaka huu sisi tukiwa na GDP ya dola Bilioni 62 watakuwa na GDP ya dola 107 sisi 62 GDP per capital ya Kenya mwishoni mwa mwaka huu itakuwa dola 1550 sisi ni dola 990. Kwa hiyo ukichukua yale magroup yaliyotengwa na World Bank jirani yetu Kenya ambaye tunataka na kumpa gesi yetu yeye yuko kwenye group la lower middle income Capita Country ambayo inaanza dola 1046 hadi 4095.
"Sisi tuko chini tuko 990, Kenya wako 1550, kwa hiyo Mheshimiwa Mwenyekiti haya tunayoanza kuyajadili leo mapendekezo yangu ni haya,"amesema.
Prof.Muhongo amefafanua kuwa, "Malengo yetu lazima tupunguze mfumko wa bei, mpango na bajeti yetu, Mwenyekiti mfumuko Agosti, mwaka huu ilikuwa 4.6 asilimia,Septemba 4.8 asilimia. Hii lazima tupunguze ndio tiyajadili tuishawishi wizara ipunguze.
"Lango la pili kwenye mipango tunayopanga na bajeti yake na inafanyika duniani kote, wamepunguza low inflation halafu wanapunguza interest rate ikiwa inflation itapanda inamaanisha mabenki nayo yatapandisha riba zao za mikopo. Kwa hiyo huu mpango na bajeti yake lazima tulenge huko.Kwamba, interest rate huko zisipande, zikipanda hata waliokopa nyumba, baiskeli, magari lazima zipande.
"Kingine ambacho tunapaswa kukiongelea kwenye hii bajeti ni kuzuia government bonds, hati fungani, kutumika pasipo kuwa na malengo sahihi maana yake ukiitumia interest ikiongezeka utalazimika kutumia hizi hati fungani. Ukishatumia ujue unaleta matatizo kwenye uchumi wa nchi.
"Kwa hiyo hii nayo bajeti ituelekeze namna ya kuzuia kukimbia kutumia government bonds, kututoa kwenye matatizo ambayo tunaweza kuyatatua kwa kutumia njia nyingine kabisa. Vile vile mpango tunayoijadili na bajeti yake lazima ituelekeze ambako wachumi wanatuelekeza.
"Kuna wachumi aina mbili na ni lazima ujue unapenda kumsikiliza nani kuna wale waliosoma Econometrics kama kina marehemu Prof. Rweyemamu na kitabu chake cha miaka 70 na kuna wale Political Economist hao maneno ni mengi na hesabu zao ni kutoa na kujumuisha tu. Sasa inabidi sijui unataka kumsikiliza yupi.
"Ukichukua wataalam wa uchumi kabisa duniani, wanasema ukitaka kupunguza uchumi lazima uchumi wako ukue kwa zaidi ya asilimia 8, kwa hiyo huu mpango lazima itueleze sababu mwaka 2020 uchumi ulikua kwa asilimia 2, mwaka jana 4.5, na mwaka huu tunategemea kwenda kati ya asilimia 4 na 5.
"Na mimi takwimu zangu waheshimiwa wabunge nazitoa kwenye vyanzo ambavyo Dunia inaviamini. Unaweza kuwa na vyanzo vyako kama huko duniani hawakijui sipendi kukitumia hicho, sasa China ukisikia kufanikiwa kiuchumi kwa zaidi ya miaka 20. Uchumi wao ulikuwa kwa kadri ya asilimia 15-20 kwa miaka 20 China ikafika hapo ilipo sasa.
"Sisi tunataka tufike tu asilimia nane growth kwa hiyo mapendekezo yangu ni haya, ukuaji ili uende kasi ndugu zangu lazima tuwe na bidhaa nyingi mpya katika soko sio kuongeza tozo. Tozo na kodi hazikuzi uchumi kinachokuza uchumi ni bidhaa kwenda kwenye soko la ndani na nje. Kwa hiyo mipango yetu na bajeti lazima itueleze hivyo.
"Halafu lazima itueleze ajira mpya sio zilezile, ajira mpya ni zipi? Na kiasi gani? Itueleze mzunguko mkubwa na mpana wa fedha kwa Wwnanchi wetu.
"Kwa hiyo tufanye yafuatayo, mimi mapendekezo yangu ni wataalam twende kwenye kilimo kina asilimia 30 ya GDP yetu hebu tupigane tufikie asilimia 40 sasa sitaki kurudia haya, haya nilishayaongea mazao ambayo lazima tuyawekee mkazo ni yale ambayo tunatumia ndani na nje ya nchi, yana soko ni mahindi, mchele, ngano, mihogo, mbogamboga na matunda haya yote matumizi yake duniani ni asilimia 40 na 60 twende huko.
"Cha pili, uvuvi na ufugaji, samaki watoke ziwani na baharini tuongeze nyama na maziwa hapa tukazane uchangie angalau asilimia 5 ya GDP yetu. Cha tatu madini tuendelee Tanzanite, dhahabu, almasi tuendelee, lakini kama nilivyokwisha kuwaeleza hapa kuna madini ambayo ni muhimu yanathamani kuliko haya. Na haya lazima mpango na bajeti hii itueleze inavyoiwezesha Geological Survey haya madini yatapatikana kwa kutumia Geological Survey sio Tume ya Madini.
"Tume ya Madini inasimamia madini, sasa utasimamiaje huna kitu kipya? Tuwapatie Geological Survey waendeleze kufanya utafiti na haya madini ni electronic industry yanayotumika kwenye electronics. Kuna paradium, rithium, copper, tin, nikel, gold, aluminum, kompyuta zote tunazotumia zina calcium na madini mengine.
"Kuna ugomvi mkubwa sasa hivi unaendelea wa micro chip kati ya Marekani na China kama mnafuatilia sababu hizi micro chips hata hizi simu zenu zote zina micro chips, kompyuta zote zina electronics zote madini yanayopatokana humo ni cilicone na layer earth element, sasa haya madini Mwenyekiti atakayetusaidia kuyapata ni Geological Survey.
"Wawekeze, wafanye utafiti watafute madini mapya yanayopatikana duniani yanaitwa 'technology metals' sasa hapa madini tujipange hadi tufikishe asilimia 15 ya GDP wanakaribia asilimia 10, lakini uchumi wetu uwasukume twende kwenye asilimia 15 ya GDP.
"Kingine ambacho ni muhimu ukiona katika mapendekezo yangu ambayo nimeanza na ajira ya watu naenda napungua ajira kilimo uvuvi ufugaji mining yote hayo yalitushinda. Tukadhani uchumi wa gesi utatutoa, lakini tukaweka kapuni sijui kama tutasalimika tusipoutoa kapuni huko.
"Ni kwamba uchumi wa gesi una vitu vitatu muhimu tutazalisha umeme mwingi wa bei nafuu na ujenzi wa mitambo yake ni wa haraka, halafu umeme wa gesi hauna jua, ukame tuta export LNG tunayotaka kuijenga pale Lindi ni biashara kubwa na tatu muhimu kabisa Petro chemical Industries. Hapa ndugu zangu waheshimiwa wabunge kabla hatujamuuzia mtu mwingine jirani yetu yeyote tunayeshindana naye gesi.
"Lazima tujiulize je, tukimpa gesi yetu yeye atakuja haraka na viwanda atuuzie bidhaa zinazotokana na gesi yetu hilo ni swali la muhimu sana.
"Petro Chemical Industries ni muhimu sana, mfano ni mbolea, viti vyote tunavyokalia, plastiki zote, sabuni na kadhalika viwanda ni vingi sana vya gesi, kwa hiyo napendekeza hapa hapa hii gesi ecomomy ituchangie kati ya 15 hadi 20 asilimia ya GDP," amefafanua Mheshimiwa Prof.Muhongo.
Tags
Bungeni
Fedha na Uchumi
Fursa za Kiuchumi Tanzania
Habari
MAENDELEO JIMBONI
Makala
Manispaa ya Musoma
Musoma Vijijini