NA DIRAMAKINI
NOVEMBA 19, 2022 wadau mbalimbali wamempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuimarisha demokrasia na kudumisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa ndani ya uongozi wake.
Wametoa pongezi hizo kupitia mkutano wa Zoom ulioratibiwa na Watch Tanzania na kurushwa na vyombo mbalimbali vya habari huku ukiongozwa na mada iliyohusu TATHIMINI YA UONGOZI WA RAIS DKT.HUSSEIN ALI MWINYI KATIKA DEMOKRASIA ZANZIBAR NA KUDUMISHA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA. Washiriki wamesema;
BARAKA SHAMTE, MWANASIASA MKONGWE
"Rais Mwinyi amejitahidi kuhubiri sana kuhusu umoja na kudumisha amani baina ya Wazanzibari ingawa kulikuwa na vipingamizi vidogo vidogo ila kwa juhudi za Rais wetu na wasaidizi wake nchi imefanikiwa kuwa na amani na utulivu.
"Rais Mwinyi amewasaidia sana wajasiriamali wadogo wadogo hasa wakulima wa mwani ameweza kuwapa vifaa mbalimbali na bei za kuuza zao hilo kuwa zuri kuliko hapo mwanzo;
JOYCE SHEBE, MWENYEKITI TAMWA
"Hapo nyuma watoto wa kike kubakwa na kulawitiwa ilikuwa ni kero kubwa sana, hivi sasa tatizo hili halipo tena hii ni juhudi za Mhe.Rais kutetea na kuwa makini katika kulitafutia suhulu hii tatizo la ubakaji na ulawiti.
"Rais Mwinyi alisema tangu mwanzo kwamba atashughulikia hili tatizo la ubakaji na ulawiti ndio maana alianzisha mahakama maalum ambayo haina zamana kwa mtu ambaye atabainika amehusika moja kwa moja kufufanya kitendo hicho cha ukatil;
DEODATUS BALILE, MWENYEKITI TEF
"Kupitia mikutano ya waandishi wa habari na Rais, ilimfanya Rais kwenda Kojani ambako hakuwahi kwenda Rais kwa kipindi cha miaka 30 na zaidi, lakini Rais Mwinyi amefanikiwa kwenda na kuwasikiliza wananchi wale na kutatua changamoto zao.
"Rais Mwinyi alipoingia madarakani ameweza kurudisha vikao vya kila mwezi yaani Rais kukutana na wahariri na waandishi wa habari pale Ikulu na kila mara tukishiriki hii mikutano tunapata fursa ya kumfikishia moja kwa moja hoja kutoka kwa wananchi;
HASSANI KIJONGOO, WAKILI WA KUJITEGEMEA
"Kwa kweli tunamshukuru sana Mhe.Rais kujitahidi kushirikisha vijana katika maslahi ya utawala bora, katika teuzi nyingi tunazoziona tunamuona Rais anajitahidi kuchagua vijana zaidi ndio maana kuna kauli huwa anapenda kusema kwamba vijana ni taifa la leo.
"Mhe.Rais ametengeneza mazingira sahihi ya kumsikiliza wananchi kutoka kila mahali, Rais wetu anatumia njia mbalimbali kuwafikia watu wake ikiwemo mikutano ya hadhara, mikutano ya ndani, mitandao ya jamii na kupitia wasaidizi wake;
JUMA KHATIBU, MWENYEKITI ADA-TADEA
"Upinzani wa vyama sio uadui, upinzani ni kuweza kuisaidia serikali pale ambapo inapotoa ahadi kwa wananchi wake na kuisaidia kuikumbusha na sio kuitusi kama viongozi wa serikali hasa vyama pinzani wanavyofanya.
"Pamoja na changamoto zote za kidunia Rais Mwinyi amefanikiwa kuiweka nchi katika hali ya umoja, amani na utulivu pia kuinyanyua Zanzibar kiuchumi, hili ni japo jema na la kupongeza kabisa;
JOSEPH MEZA,MAKAMU MWENYEKITI JITEGEMEE CO.LTD
"Kwa mujibu wa Kanuni na Sheria za nchi Rais ndie kiongozi Mkuu wa Nchi hivyo ukiwa na jambo lolote katika kumshauri Rais unapaswa kufuata kanuni na taratibu, kinyume chake ni kumvunjia heshima na kukiuka taratibu za nchi.
“Tabia zetu ni kuheshimu viongozi na watu wazima na kama unamshauri ni kupitia taratibu za kiheshima sio kutoa amri mitandaoni. Inasikitisha sana kuona chama ambacho kina kiongozi mkubwa tu katika Serikali kinakurupuka kwenye mitandao kutoa maagizo kwa kiongozi mkuu wa nchi badala ya kumtumia yeye kwa kupeleka ushauri au maoni;
LEILA NGOZI, MJUMBE WA KAMATI KUU YA TAIFA (CCM)
"Kumekuwa na kasumba ya vyama vya upinzani wakiitwa jina hilo basi kunakuwa na uadui kati ya chama tawala na vyama pinzani, hii haipo sawa vyama vya upinzani vipo nchini kikatiba sio kwa ajili ya kuwa adui bali ni wasaidizi wa serikali pale jicho la serikali halioni vizuri.
"Bahati nzuri mwenye macho haambiwi tazama kila kitu kipo wazi katika maendeleo yanaonekana, uchumi unaimarika achilia mbali changamoto za kidunia ya vita na magonjwa;
JUMA MOHAMMED, MWANAHABARI NA MTANGAZAJI
AMEIR HASSAN AMEIR, KATIBU MKUU CHAMA CHA DEMOKRASIA MAKINI
"Mimi nachukua fursa hii kumpongeza Rais kwa kazi kubwa ambayo anaifanya ili kuhakikisha Wazanzibari wanapata maendeleo, wito wangu kwake aendelee kutekeleza dhamira yake njema kwa Wazanzibari.