Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali leo, kuapishwa Ikulu kesho

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 10, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Islam Seif Salum kuwa Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Kabla ya uteuzi wa Dkt.Islam alikuwa Katibu Mkuu (Kazi na Uwezeshaji) katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Maryam Juma A.Saadalla kuwa Katibu Mkuu (Kazi na Uwezeshaji) katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji. Kabla ya uteuzi Maryam alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Ali Khamis Juma kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda. Kabla ya uteuzi, ndugu Ali alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Abeida Rashid Abdallah kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Kabla ya uteuzi huo, Abeida alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Tano, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Khamis Abdulla Said kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali. Kabla ya uteuzi huo, Khamis alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Sita,Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Saleh Juma Mussa kuwa Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais-Ikulu. Kabla ya uteuzi huo, Saleh alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-Ikulu.

Saba, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Thabit Idarous Faina kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Uchaguzi. Kabla ya uteuzi huo, Thabit alikuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Wakati huo huo, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said amebainisha kuwa, uteuzi wa Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi kwa viongozi hao umeanza leo Novemba 10, 2022.

Pia, wateuliwa wote waliotajwa wataapishwa kesho Ijumaa ya Novemba 11, 2022 saa 4:00 asubuhi Ikulu jijini Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news