Rais Dkt.Mwinyi:Ushirikiano wa pamoja katika huduma za macho Zanzibar ni muhimu

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina wagonjwa wengi wenye matatizo mbalimbali ya macho, hivyo misaada kutoka taasisi za ndani na nje ya nchi ni muhimu.
Dkt.Mwinyi amesema hayo wakati alipozungumza na kikundi cha madaktari kutoka Taasisi ya ‘Association Vission-for-Puma (Germany) kilichoongozwa na Dkt.Frank Klemm, kilichofika Ikulu Zanzibar baada ya kumaliza zoezi la utoaji wa huduma na tiba ya macho katika Hospitali ya KMKM Kibweni, Mkoa Mjini Magharibi Unguja.

Dkt.Mwinyi amesema pamoja na Zanzibar kuwa na Hospitali ya macho katika Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja, bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa vifaa muhimu pamoja na wataalamu, mambo yatakayofanikisha utoaji bora wa huduma za macho nchini.

Ametumia fursa hiyo kuipongeza timu ya madaktari hao kwa ujio wao pamoja na kazi kubwa waliyofanya ya kuwapatia huduma mbalimbali wagonjwa.

Amesema serikali itaangalia namna ya kuendeleza ushirikiano ulioanza na taasisi hiyo katika siku zijazo.

Naye Kiongozi wa timu hiyo ya madaktari kutoka Taasisi ya ‘Association Vission –for-Puma (Germany), Dkt.Fank Klemm alipongeza ushirikiano mkubwa waliopata kutoka Uongozi wa Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) pamoja na madaktari wa Hospitali ya KMKM Kibweni katika kipindi chote walipokuwa nchini.

Amesema, wagonjwa 100 walipatiwa huduma mbalimbali za macho katika kliniki hiyo iliodumu kwa siku 12, huku wengine wakipatiwa miwani ya macho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news