NA MWANDISHI WETU
HATIMAYE RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekabidhiwa Tuzo ya Uongozi wa Kimageuzi barani Afrika (African Leadership Award 2022) kutoka Taasisi ya Afrimma ya mjini Dallas, Marekani kwa kutambua mchango wake katika sanaa nchini Tanzania.

Awali mamia ya mashabiki waliohudhuria tuzo hizo walimshangilia kwa nguvu Rais Samia alipoonekana katika baadhi ya vipande vya filamu ya Royal Tour vilivyokuwa vikioneshwa kabla ya kutolewa tuzo hiyo.
Viongozi wengine wakuu wa Afrika waliowahi kutwaa Tuzo hiyo ni Rais Ian Khama wa Botswana (2015) na Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria (2017).