1. SERA YA MAMBO YA NJE:-Rais Samia amefanikiwa kurudisha heshima ya Tanzania kimataifa kwa kudumisha mashirikiano yenye tija na kushiriki kikamilifu katika agenda za kimataifa zenye faida si tu kwa Tanzania bali kwa Afrika na Dunia kwa ujumla.
2. UWAZI NA UWAJIBIKAJI:-Rais Samia amefanikiwa kuzipa taasisi serikali na mashirika ya umma uhuru wa kuwajibika na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria ili kuongeza ufanisi. Hii imewezesha kutolewa ajira, kulipa malimbikizo, madeni, kupandisha watumishi madaraja na nyinginezo bila urasimu.
3. UTAWALA WA SHERIA:-Rais Samia amefanikiwa kuupa muhimili wa Mahakama uhuru wa kufuata sheria katika utoaji haki na kuondoa kesi za kisiasa kwenye mahakama ili kudumisha misingi ya utawala wa sheria na utoaji haki.
4. KUBORESHA HUDUMA KIJAMII:-Rais Samia anaendelea kufanikiwa kwa viwango vya juu katika kuboresha huduma za jamii. Mpaka sasa elimu inatolewa bure kwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha Sita na Mikopo ya Elimu ya juu kwa wote wenye sifa.
5. KUSIKILIZA MAONI NA USHAURI:-Rais Samia amefanikiwa kutengeneza mazingira huru kwa wananchi kutoa mrejesho juu ya mambo mbalimbali na kutoa ushauri katika mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yao. Sifa hii ni ya kipekee sana kwa viongozi.
6. UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI:-Rais Samia amefanikiwa kusimamia miradi kwa kufuata taratibu zinazoweza kutoa matokeo chanya badala ya mbwembwe zisizo na tija. Sifa hii ndio msingi wa mafanikio katika miradi mingi ambayo inampa faraja kila mtanzania mwenye akili timamu.