NA ASILA TWAHA,OR-TAMISEMI
TIMU ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ngazi ya Mkoa ( RHMT) imeshauriwa kuwa na tabia ya kutumia chumba cha kuchakata takwimu ( Situation Room) ili kufanya maamuzi sahihi yatakayopelekea uboreshaji na uimarishaji wa huduma za afya nchini.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 10, 2022 jijini Dodoma katika mafunzo ya kutumia takwimu katika chumba cha uchakataji ( Situation room) kwa RHMT Mkoa wa Dodoma.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Ufundi Mradi wa Data For Implementation Bw.Jackson Ilangali ambae amesema kuwa ili kuleta matokeo chanya katika sekta ya afya lazima kutumia taarifa na takwimu sahihi ambazo zinaendana na uhalisia wa huduma inayotolewa pamoja na wananchi wanaopata huduma hiyo.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo RHMT jinsi ya kutumia chumba cha uchakataji takwimu ( SITUATION ROOM) katika kufanya maamuzi sahihi ili kuendelea kuboresha utolewaji wa huduma za afya kwa wananchi.