NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inafanya mapinduzi makubwa katika kuboresha usafiri wa majini kwa kujenga meli na kusomesha wataalam anuai wa fani ya bahari.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akimkabidhi cheti cha pongezi Katibu Mtendaji wa Kwanza wa Taasisi ya Ushoroba wa Kati (CCTTFA), Bi. Rukia Shamte katika Mahafali ya Kwanza ya wanafunzi wa fani ya Ubaharia jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kozi ya ubaharia ambayo yamefadhiliwa na Taasisi ya Ushoroba wa Kati (CCTTFA) jijini Dar es Salaam amewataka wahitimu wa kozi hiyo, kuwa na nidhamu ili ujuzi walioupata uwe na manufaa kwa taifa na nchi za ushoroba wa kati kwa ujumla.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Wahitimu wa Mahafali ya Kwanza ya wanafunzi wa fani ya Ubaharia yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Ushoroba wa Kati (CCTTFA), yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Baharia mzuri ni yule mwenye nidhamu anapokuwa akitekeleza majukumu yake, maono na anayezingatia usalama wake, chombo na mali kwa ujumla,” amesisitiza.
Aidha amekitaka Chuo cha Bahari (DMI) kuhakikisha kinakuza mtandao wake na taasisi mbalimbali duniani ili kuwawezesha wanafunzi wa chuo hicho kupata muda wa kutosha wa kufanya mazoezi ya vitendo melini (Sea time).
Wahitimu wa Mahafali ya Kwanza ya fani ya Ubaharia yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Ushoroba wa Kati (CCTTFA), wakiwa kwenye hafla ya mahafali yao jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Prof. Makame ameupongeza wakala wa ushoroba wa kati kwa kuwafadhili wanafunzi hao na kuahidi kutilia mkazo wa kuwa na mpango unaotekelezeka wa mafunzo kwa vitendo.
“Serikali tunajukumu kubwa la kuhakikisha wanafunzi wetu wa fani za bahari wanapata mafunzo kwa vitendo ya kutosha (Sea time) ili kuwaongezea ujuzi, kwenye utekelezaji wa kazi zao".
Waziri wa Miundombinu wa Burundi, Captain Dieudonne Dukundane akizungumza kwa Wahitimu wa Mahafali ya Kwanza ya wanafunzi wa fani ya Ubaharia yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Ushoroba wa Kati (CCTTFA), yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Waziri wa Miundombinu wa Burundi, Captain Dieudonne Dukundane ameipongeza Tanzania kwa kutumia rasilimali zake katika kuhakikisha wahitimu wa nchi zote za ushoroba wa kati wanasoma na kuhitimu salama, na kusisitiza wahitimu hao kuwa wazalendo na kufikia malengo ya kuhimarisha huduma za usafiri majini.
Amezungumzia umuhimu wa nchi Wanachama wa Ukanda wa ushoroba wa Kati kutekeleza program walizojiwekea za kuimarisha usafiri na usafishaji hususani katika bahari na maziwa ili kukuza uchumi wa nchi zoTE.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akimkabidhi cheti cha kumaliza mafunzo ya ubaharia, Bi. Radhia Sosovele katika Mahafali ya Kwanza ya wanafunzi wa fani ya Ubaharia yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Ushoroba wa Kati (CCTTFA) jijini Dar es Salaam.
Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari DMI, Dk. Tumaini Gurumo amesema wahitimu hao wamepata mafunzo stahiki ambayo yatawawezesha kufanya kazi katika nchi zote zenye bahari na maziwa duniani.
Pamoja na hayo amezungumzia umuhimu wa kuwa na meli zinazomilikiwa na nchi wanachama wa ukanda wa ushoroba wa kati ili kuimarisha mazoezi ya vitendo kwa mabaharia.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa nchi wanachama wa ushoroba wa Mahafali ya Kwanza ya wanafunzi wa fani ya Ubaharia jijini Dar es Salaam.
Jumla ya wanafunzi kumi kutoka nchi wanachama wa Ushoroba wa Kati, ambazo ni Rwanda, Burundi, Uganda, DRC Kongo na Tanzania.