TANZANIA YASHUKURU SHIRIKISHO LA JUDO ULIMWENGUNI

NA ADELADIUS MAKWEGA-WUSM

SERIKALI imekipongeza Chama cha Mchezo wa Judo nchini kwa utendaji wake bora, kwani kwa muda mfupi kimefanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji.

Hivyo, itaendelea kuwa nacho bega bega kufanikisha mara dufu mafanikio ya mchezo wa huo ili kwenda na dhamira ya Serikali ya Awamu Sita katika kuinua michezo nchini.
Hayo yemesema leo Novemba 30, 2022 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini ndugu Said Yakub wakati alipotembelewa na Rais wa Mchezo wa Judo nchini ndugu Zaidi Hamisi wizarani hapa Mtumba Mji wa Serikali jijini Dodoma.

“Mmeainisha mambo mengi ya muda mfupi na ya muda mrefu, jambo la msingi Chama cha Judo lazima kiwe taasisi kamili, yenye mipango ya muda mrefu, muwe na mpango mkakati wa miaka mitano, muwe na kituo cha mafunzo, hapo litakuwa eneo ambalo mafunzo ya mchezo huo yatafanyika. Serikali itaratibu ufundishaji wa Judo mashuleni kwa ushirikiano na wizara zinazosimamia shule zetu. 

"Tunamshukuru Rais wa Shirikisho la Judo Ulimwenguni ndugu Marlus Vizer kwa kutoa msaada wake kwa michezo huo na tunamualika aje Tanzania kukutana na viongozi wa michezo nchini,"amesema.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Naibu Katibu Mkuu Yakub alipigia chapuo Chama cha Mchezo wa Judo kupewa vyumba vya kuchezea mchezo huo katika viwanja vya michezo nchini, hilo alimuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini ndugu Ali Mayay Tembele kulitekeleza.

Akizungumza katika kikao hicho, Rais wa Mchezo wa huo ndugu Hamisi alipokea pongezi hizo kwa mikono miwili akisema kuwa Tanzania itapokea jozi 50 ya nguo za mchezo wa judo katika mashindano ya kimataifa, jozi 100 za nguo za mafunzo ya mchezo huo na pia jozi 200 za nguo mazoezi kwa ajili ya wanafunzi na pia Tanzania itapata nafasi ya kusomeshewa walimu wa mchezo huo kwa ngazi ya shahada.

Judo ni mchezo wenye asili ya Japan huku ukichezwa sana katika mataifa ya Bara Ulaya ikiwamo Ufaransa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news