NA LWAGA MWAMBANDE
WENGI wetu tunatambua kuwa, ugoro ni tumbaku ambayo ipo katika mfumo wa unga baada ya kusagwa ambapo siku za karibuni makundi mbalimbali ya watu wakiwemo vijana na wazee wamekuwa wakiitumia kwa kuilamba au kuinusisha puani.
Makundi hayo, wengi wamekuwa wakiutumia ugoro huo pengine kwa kufahamu au kutofahamu madhara hasi kiafya.
Licha ya kujiona kuwa wanajistarehesha, wataalam wa afya mara zote huwa wanasisitiza kuwa, matumizi ya iwe ugoro, sigara au dawa zozote za kulevya yana madhara mengi kiafya.
Makundi hayo, wengi wamekuwa wakiutumia ugoro huo pengine kwa kufahamu au kutofahamu madhara hasi kiafya.
Licha ya kujiona kuwa wanajistarehesha, wataalam wa afya mara zote huwa wanasisitiza kuwa, matumizi ya iwe ugoro, sigara au dawa zozote za kulevya yana madhara mengi kiafya.
Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasema kuwa, ili kuweza kuishinda nguvu ya ushawisi inayokupa hamasa kutumia vitu hivyo ukiwemo ugoro yafaa kujitenga au kuvitupilia mbali vitu vyote ambavyo huwa vinakufanya ujiwekee akiba ya baadaye ikiwemo tabakero, endelea;
1. Huutumii ugoro,
Tupa hilo tabakero,
Kwako lisiisiwe ni kero,
Urudie kubugia.
2. Kivutio tabakero,
Kwako mvuta ugoro,
Mwilini hiyo kasoro,
Kuvuta utarudia.
3. Ulishuka hadi ziro,
Kuacha vuta ugoro,
Kuiona tabakero,
Kama wataka rudia.
4. Toka kufikia ziro,
Kutumikia ugoro,
Kukohoa siyo kero,
Vile ilikuzidia.
5. Sasa hiyo tabakero,
Kuwepo hapo kasoro,
Tataka tunza ugoro,
Kunusa utarudia.
6. Tumba mbali tabakero,
Kama imetiwa sero,
Uongeze mdororo,
Ugoro kutotumia.
7. Hawa wavuta ugoro,
Benki yao tabakero,
Humo wajaza ugoro,
Wazidi kujivutia.
8. Wakitupa tabakero,
Hawataona ugoro,
Magonjwa na zake kero,
Kwao zitawaishia.
9. Sawa sigara ugoro,
Athari zake ni kero,
Ukitupa tabakero,
Kuvuta kutaishia.
10. Harufu yake ni kero,
Na tena kubwa kasoro,
Hata magonjwa ni kero,
Waugua waishia.
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602