NA DIRAMAKINI
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ameungana na vijana wa Lindi kufanya usafi maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Lindi ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye atawasili mkoani humo kesho Disemba 1, 2022.
"Sisi Vijana wa Lindi ilifikia hatua baadhi ya wanasiasa walituita watoto tuliotengwa, lakini walisahau licha Mkoa wa Lindi kutotembelewa na Rais kwa muda mrefu Mama yetu Samia Suluhu akiwa Makamu wa Rais alitutembelea sana,"amesema Mustafa Dumbo kwa niaba ya Vijana wa Lindi.
"Hivyo basi sisi vijana wa Lindi mbele ya Rais hatujihisi tuliotengwa kwa sababu alikua anatupenda kabla ya kuwa Rais wa nchi lakini hata sasa Mama Yetu ameendelea kuonesha upendi kwetu kwa kutupa vijana nafasi za ajira za Watendajinwa Kata, ametupa mikopo ya Halmashauri na Mikopo ya Bodaboda,"ameongeza Mustafa Dumbo.
Akiwajibu vijana Waziri Nape Nnauye amewataka vijana hao kutambua Rais Samia anawapenda sana mkoa wa Lindi.