Wachezaji sita tegemeo KMC FC wakabiliwa na majeraha

NA DIRAMAKINI

TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC) jijini Dar es Salaam inakabiliwa na changamoto ya wachezaji sita tegemeo ambao ni majeruhi ndani ya kikosi hicho ambapo kwa sasa wanaendelea na matibabu.
Wachezaji hao ni Hance Masound ambaye aliumia jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars na hivyo kushindwa kuendelea jambo lililopelekea kukimbizwa hospitali na gari la wagonjwa.

Christina Mwagala ambaye ni Afisa Habari na Mawasiliano KMC ameyabainisha hayo leo Novemba 24, 2022.

Wachezaji wangine ambao jana walishindwa kuendelea na mchezo mbali na Hance Masound ni Ibrahim Ame, Baraka Majogoro ambao pia kwa nyakati tofauti katika mchezo huo uliomalizika kwa KMC FC kupoteza kwa bao moja ugenini walishindwa kuendelea na mchezo kutokana na kupata majeraha.

Aidha,Mwagala amesema wachezaji wengine ni Kelvin Kijili, Awesu Ally Awesu pamoja na Emmanuel Mvuyekure ambao hawa pia walikuwa na majeraha ya muda mrefu hali iliyopelekea kushindwa kusafiri na timu kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars.
"Kwa sasa tunakabiliwa na changamoto kubwa ya wachezaji wenye majeraha, na ukiangalia kwenye timu kila mchezaji ana mchango mkubwa pindi anapopewa majukumu na kocha, hivyo nikipindi kigumu lakini tutajitahidi kadiri tuwesavyo ili kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja,"amesema.
Katika hatua nyingine KMC FC imerejea jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo ikitokea mkoani Singida na kesho itaanza kufanya maandalizi kuelekea katika mchezo unaokuja dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Novemba 28, 2022 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news