Wafanyakazi waliofanikisha Kombe la Dunia sasa wanafurahia matunda ya kazi zao

NA DIRAMAKINI

BAADA ya msoto wa kazi ngumu, sasa umewadia wakati wa shangwe. Jijini Doha nchini Qatar furaha imetanda huku maelfu ya wafanyakazi wahamiaji wakijitokeza kutazama mchezo wa kwanza wa kihistoria wa Kombe la Dunia la FIFA 2022 lililoshirikisha Qatar na Ecuador kwenye Eneo la Mashabiki wa Eneo la Viwanda katika mji mkuu wa Qatar, Doha.

Wafanyakazi hawa walikusanyika kutazama mechi ya ufunguzi ya Qatar dhidi ya Ecuador katika Eneo la Mashabiki wa Eneo la Viwanda huko Doha, Qatar, Novemba 20, 2022. (Picha naMarko Djurica/Reuters).

Takribani wanaume wote, umati uliojaa wa wafanyakazi wengi wa Asia Kusini kutoka India, Bangladesh, Pakistan na Nepal, pamoja na wengine kutoka Afrika, walikuwa wamesaidia kujenga miundombinu iliyoruhusu Kombe la Dunia kufanyika.

Madai ya wasiwasi kuhusu mishahara duni, hali duni ya maisha na masuala ya usalama wa wafanyakazi nchini Qatar yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na makundi ya haki za binadamu na wakosoaji wa taifa hilo la Ghuba kuandaa Kombe la Dunia.

Ukosoaji huo ulisababisha mageuzi mwaka 2020, ikiwa ni pamoja na Qatar kufuta kile kinachoitwa cheti cha kutopinga maamuzi, ambacho kiliwalazimu wafanyakazi kutafuta ridhaa kutoka kwa waajiri wao wa sasa kabla ya kuruhusiwa kubadili kazi. Qatar pia imeanzisha kima cha chini cha mshahara kwa mwezi cha riyal 1,000 za Qatar ($275).

Mbali na hayo, wachakarikaji hao Siku ya Jumapili jioni, walikuwa tayari zaidi kufurahia mchezo na kuthamini matunda ya kazi yao.

Wengine walifika wakiwa na ovaroli zao za kazi baada ya kutoka kazini moja kwa moja. Wengine walikuwa na siku ya mapumziko, na kuna wale ambao walikuwa wamewauliza waajiri ikiwa wangeweza kuacha kazi ili kutazama mechi.

"Hapa, niko katikati yake ... na kwa kawaida nimefurahishwa sana," Muhammad Hossein mwenye umri wa miaka 45 kutoka Bangladesh aliiambia Al Jazeera katika eneo la mashabiki katika Uwanja wa Kriketi wa Jiji la Doha.

"Kuwa sehemu ya Kombe la Dunia lilikuwa jambo kubwa kwangu binafsi na pia,kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza kwa nchi ya Kiislamu kuandaa mashindano haya,"amesema ingawa hakuwahi kufikiria kama angekuwa sehemu ya kitu muhimu sana katika ukanda huo.

Ingawa nchi yake ni mojawapo ya mataifa makubwa yanayocheza kriketi duniani, Hossein anaonekana kutokuwa na matumaini na taifa lake la Bangladesh katika soka la Kimataifa.

Qatar, ambayo ina wakazi wapatao milioni 2.8 tu, imekuwa nchi ya kwanza ya Mashariki ya Kati na Kiislamu kuandaa Kombe la Dunia la FIFA.

Maandalizi ya miundombinu na huduma nyinginezo katika Taifa hilo kwa ajili ya Kombe la Dunia 2022 yametegemea zaidi nguvu kazi ya wafanyakazi kutoka nje ya nchi.

"Qatar haikuwa na mabasi unayoyaona barabarani. Majengo haya yote unayoyaona, barabara kuu na barabara labda zisingekuwepo ikiwa tukio hili kubwa halingefanyika,” Peter, mfanyakazi kutoka India, aliiambia Al Jazeera.

"Nina furaha kusema sisi (wafanyakazi wahamiaji) tulichukua jukumu kubwa," alisema kijana huyo mwenye umri wa miaka 48, ambaye alikuja Qatar zaidi ya miaka 15 iliyopita na kufanya kazi katika kampuni ya kutengeneza nyuzi.

Wakati huo huo, Novemba 20, 2022 timu ya Taifa ya Ecuador ilikuwa ya kwanza kujizolea alama tatu zikisindikizwa na mabao mawili katika michuano ya Kombe la Dunia 2022 inayoendelea nchini Qatar

Ni baada ya kuwapiga mabao mawili wenyeji kupitia mtanange wa moto na wa ufunguzi uliopigwa katika Dimba la Al Bayt Stadium lililopo Al Khor, Qatar.

Mshambulizi wa Fenerbahce, Enner Valencia aliifungia Ecuador bao la mapema dakika ya tatu kabla ya mwamuzi msaidizi wa video (VAR) kulikataa.

Valencia aliweka mpira tena langoni mwa Qatar, kwa mkwaju wa penalti, dakika ya 16, na kisha dakika ya 31, akafunga tena kwa kichwa.

Aidha, licha ya uchezaji bora wa Qatar baada ya bao la pili la Ecuador na Almoez Ali kukosa mkwaju muhimu katika sekunde za mwisho. Pedro wa Qatar alipoteza nafasi nyingine muhimu ya bao dakika ya 61. Baada ya shuti la mbali la Muntari wa Qatar kuzikosa nyavu za Ecuador kwa dakika ya 85, mchezo ulimalizika kwa Ecuador kwa mabao 2-0.

Kutokana na matokeo haya, Qatar imekuwa wenyeji wa kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kupoteza mechi ya ufunguzi.

Ecuador sasa inaongoza Kundi A la Kombe la Dunia kwa alama tatau huku Qatar ikishika nafasi ya nne kwa sifuri.Senegal itamenyana na Uholanzi katika mechi inayofuata ya Kundi A leo Novemba 21, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news