Wajawazito wafike kliniki mapema-Dkt.Mollel

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetoa wito kwa Wajawazito kuhudhuria mapema kliniki ili kutoa muda wa kutosha kwa Wataalamu kufanya uchunguzi na ufuatiliaji ili kuepusha dharura za kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel katika kikao cha tisa cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Dkt. Christina Mnzava.

Amesema, Serikali inaendelea kutimiza jukumu lake kwa kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto, hivyo kutoa wito kwa Wajawazito kujenga tabia ya hudhurio kliniki na kufanyiwa uchunguzi ili kujua hali zao mapema.

Aidha, Dkt. Mollel amesema, Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi, hususan wajawazito kupata lishe bora ili kujenga mtoto mwenye afya njema na kumlinda dhidi ya magonjwa.

Akijibu swali la Dkt. Alice Kaijage kuhusu upungufu wa Wataalamu wa mazoezi tiba na utengamao Dkt. Mollel amesema, Serikali imeajiri jumla ya Wataalamu 84 wa mazoezi tiba na huduma za utengamao katika ajira za mwezi Julai 2022 na hivyo kufanya idadi ya wataalamu wa mazoezi tiba na huduma utengamao kuongezeka kutoka 653 hadi 737.

Kwa sasa kuna jumla ya vyuo vikuu vinne (Muhimbili, KCMC, Bugando na Zanzibar) vinavyotoa taaluma hivyo kupunguza changamoto ya uwepo wa Wataalamu katika soko la ajira.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news