NA DIRAMAKINI
WAKULIMA wa Mkoa wa Kagera wamemuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wanasiasa ambao wamejifanya hawatambui mchango wa Serikali hasa kwenye Sekta ya Kilimo huku wakisema wengine wamekua wasomi kwa sababu wazazi wao waliwezeshwa kwenye kilimo kupitia Serikali.
Maandamano ya kumuomba msamaha Rais Samia Suluhu Hassan yameanzia Mtaa wa Miembeni hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mhe. Albert Chalamila.
"Tunakuomba sana Mkuu wa Mkoa upokee ombi letu la Msamaha sisi Wakulima wa Kagera kwa wanachokifanya watoto wetu tuliowasomesha kupitia Kilimo tulichosaidiwa na Serikali ambayo wengine wanasema tusiishukuru, tunamuomba sana Msamaha kwa niaba yake na aendelee kutufanyia mambo mazuri,"amesema Josephat Joseph Kyamuhangile kwa niaba ya Wakulima wa Mkoa wa Kagera.
Kwa upande wake Mkuu wa Kagera,Mhe. Albert Chalamila amewaeleza mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Samia kwenye Sekta ya Kilimo.